MSANII nyota
wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba amefunguka kuhusu tuhuma zinazopelekwa
kwake moja kwa moja kwamba ndiye kinara wa zomeazomea nafujo anazofanyiwa
Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Kusema kweli
mimi sihusiki na shutuma hizo dhidi yangu siyo za kweli mimi kama msanii nina
mambo mengi ya kufanya lakini siyo kumuundia genge Diamond la kumzomea na kurushia chupa.
Hayo
yalisema na Kiba alipozungumza na mwandishi wa habari hii Jijini Dar es Salaam
katika mahojiano maalum.
“Unajua
mashabiki wana mambo yao lakini binafsi sipendi kusikia wala kuona Diamond
anadhalilishwa kwenye majukwaa” alisema Kiba.
Aliongeza
kwa kusema kuwa hafurahishwi kabisa kuona hali ya msanii kudhalilishwa huku
akikumbushia katika tamasha la Tigo lililofanyika Januari 25 kwenye uwanja wa
Leaders Club ambapo Diamond alirushiwa chupa zenye haja ndogo jukwaani
akaanguka akazomewa pia.
Kiba alitoa
rai kwa mashabiki kuwacha kabisa mtindo huo kama wanampenda wampende tu lakini
siyo kumfanyia fujo Diamond.
“Mimi sina
team Kiba nasikia tu sababu siwezi kuka chini msanii mkubwa kama mimi halafu
nikapanga fujo badala ya burudani “alisema Kiba.
Kuzomewa kwa
diamond katika tamasha hilo la tigo ni mara ya pili kwani mara ya kwanza
alizomewa katika tamasha la Fiesta mwaka jana
liliofanyika kwenye uwanja huohuo wa Leaders Club.
0 Comments