KUNDI la muziki wa taarabu la Gusa Gusa
linatarajiwa kupeperusha bendera ya nchi katika onyesho litakalofanyika jijini
London nchini Uingereza Februari 7, mwaka
huu.
Kundi hilo litakwenda kunogesha maadhimisho ya
miaka kumi ya Didas Entertainment na Februari 14 watafanya onyesho katika mji wa Northampton
nchini Uingereza.
Ziara ya Gusa Gusa Mini Band imeandaliwa na
Kampuni ya Didas Entertainment yenye maskani yake nchini Uingereza.
Akizungumza kwa
njia ya simu, Mkurugenzi wa Didas Entertainment, Khadija Seif ‘Didas’,mwenye maskani yake Jijini London alisema
kwamba maandalizi yamekamilika na pia bendi ya Gusa Gusa ambayo tayari wamekamilisha
albamu yao ya kwanza inayokwenda kwa
jina la ‘Unajidodo Linakuchukucha’.
Aidha, tayari
bendi hiyo kwa sasa inatamba na vibao vyao viwili vilivyomo katika albamu hiyo
ambavyo ni ‘Unajidodo Linakuchukucha’, wimbo ulioimbwa na mwimbaji mkongwe wa
mipasho nchini, Afua Suleiman, almaarufu kama B52.
Kibao kingine kinakwenda
kwa jina la ‘Mapenzi Hayana Fomula’ kilichoimbwa na Mkongwe Sabaha Salum
Muchacho ‘Beauty Queen’.
Nyimbo zinazotarajiwa
kupakuliwa hivi karibuni ni pamoja na ‘Azurure’ utakaoimbwa na Mzee Sultan na
‘Mwanangenzi’ utaimbwa na muimbaji chipukizi, Asya Maryam.
0 Comments