MKURUGENZI wa Kampuni ya The African Stars Entertainment
(ASET),Asha Baraka na Mkurgenzi wa bendi ya Extra Bango Ally Choki, leo wamemaliza
tofauti zao katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Bamaga Jijini Dar
es salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima Asha alikiri kwamba habari
hizo ni za kweli na kwa sasa yeye na Choki hakuna chuki kati yao.
Wadau mbalimbali walitoa maoni yao katika mtandao na
kutoa ushauri kama ifuatavyo kwa wakurugenzi hawa.
Mirinda Nyeusi ambaye kwa sasa yuko nchini Duabi kikazi
alisema kwamba anasifu waili hao kumaliza bifu walilokuwa nao kwa miaka kadhaa
kwani halisaidii kitu chochote ila ni
kujivunjia njia ya mungu.
“Safi sana mama wanamuziki wote wa Tanzania pamoja na
Prezident Mzee wa Farasi” alisema Mirinda.Huku Mzee Yusuf akisema neno moja tu
Alhamdulillah.
Naye Karima Chichi Mhandeni amabye ni mdau wa muziki wa
dansi nchini alisema laiti kama angelikuwa akitumia kilevi basi leo angekunywa
kwa furaha kwani chuki siyo nzuri hata
mungu hapendi na hakuna jambo lisiloisha
mungu awajaalie awaepushe na shari za
dunia kwani wao ni wamoja na wanategemeana , kuna leo na kesho hajui atakayemuokota mwenzie tunashukuru.
Kwani
tunahitaji tuone kazi na sio
tofauti, hii hadithi inanifundisha
kuwa watu wagombanao ndiyo wapatanao .
Aidha Mwenyekuvunja undugu hataona pepo sisi sote ni ndugu , mungu awajaalie
Wakati
huohuo Lulu Kiluvia aalisema “Nisha kutana na watu hawawezagi kuweka kitu
kinyongo hua Asha baraka namba moja mtatofautiana
lakini ipo siku kwake yataisha sasa kazi kwenu mnao kuaga wapambe nuksi “
alisema Kiluvia.
Choki na
Asha Tumefurahi sana kuwaona mpo pamoja hili ni tukio zuri hata vitabu vya dini
vinasema patana na nduguyo maana hujui muda wala saa ambayo mungu atakuhitaji ,
mwenye kuupenda muziki wetu wa dansi hii ni habari njema sana kila mmoja hapo
anatambua umuhimu wa mwenzake Choki
anajua ametangaza namna gani jina lake kupitia bendi hiyo lakini kama sikosei
yeye ndiye ameshiriki album nyingi na zilizofanya vizuri sana hapo hayo Asha
lazima ayakumbuke hao watu wana mengi ya kuwafanya waheshimiane washikamane ili
zoezi linaloendelea la kuupigania muziki huu liwe na nguvu moja.
“Ally najua unanijua naitwa Championi niko Mtwara mi nashukuru saana kwa tendo hilo wote wewe na dada Asha mmefuata dini inavyotaka nimefurahi sana rudi twanga tujenge bendi
Choki”.
Maoni
yaliyotolea ni mengi kama vile wasanii ni kioo cha jamii hivyo wasimame katika
mema na umoja na ushirikiano vilevile ustahamilivu ili wengine wajifunze toka
kwao Mashabiki tusiingilie ugomvi wa wamiliki na wanamuziki, kwetu Sisi tunachohitaji
ni amani na burudani.
Choki na Asha walikuwa mahasimu bada ya Choki
kuihama Twanga na kwenda kuanzisha bendi yake
hadi kufikia kiasi cha kutopeana salamu na kuapizana wasizikane pindi mmoja kati yao atakapokufa.
0 Comments