Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa
katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi Octoba 4,
2012.
(PICHA ZOTE NA IKULU)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada
ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya
Confederation Square jijini Otttawa Alhamisi Octoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya
kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe
Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper na Spika
wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja
na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la Zanzibar (Zanzibar
chest) Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti
la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen
Harper wakiongea na wanahabari katika jengo la Bunge la Seneti la nchi
hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Gavana Jenerali wa Canada Mhe David
Johnson baada ya kuihitimisha ziara yake ya siku mbili jijini Ottawa. Baada ya
hapo alielekea jijini Edmonton ambako pamoja na shughuli mbalimbali alitarajiwa
kufungua mkutano wa Diaspora wa Watanzania wanaoishi Canada pamoja na
wawamkilishi wa makampuni na mashirika waliotoka Tanzania kuhuduria mkutano huo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Watanzania Richard Katambi Masalu na mkewe
Patricia katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa kabla ya kuondoka kuelekea
Edmonton.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(wa pili mbele kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Alex Massinda
(mbele kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makampuni ya Canada
baada ya mazungumzo katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mhe
Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi Oktoba 4,
2012.
0 Comments