Mkurugenzi wa Kampuni ya
I-View Studios, Raqey Mohammed akibadilishana mkataba na msanii Diamond
Platnumz baada ya kusaini. Wanaoshuhudia ni Mwanasheria wa Diamond, Paul Mgaya,
Mwanasheria wa I-View Dr. Peter Aringo na Mkurugenzi wa One Touch Solutions,
Petter Mwendapole.
DAR ES SALAAM, TanzaniaMSANII wa kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul
‘Diamond Platnumz’ ameingia mkataba na kampuni ya I-View Studios ya ili
wasimamie kazi zote kwa muda wa miaka miwili.
Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solution ya
mjini Dar es Salaam, Petter Mwendapole amesema I-View itasimamia mikataba yote
ya kazi zote za msanii huyo na yeyote atakayetaka kufanya kazi na Diamond kwa
sasa itabidi awasiliane I-View.
“Diamond ameamua kufanya kazi zake kimataifa, na
ameingia mkataba na I-View ambapo wao ndio watakuwa wakisimamia maonyesho,
matangazo, nyimbo kwenye simu, nguo kila kitu ambacho kinahusiana nay eye
kinapaswa kupitia I-View,” amesema.
Mwendapole alisema pamoja na maonyesho, lakini
I-View pia itawajibika katika muonekano mpya wa msanii huyo ambaye kwa sasa
anatamba ndani na nje ya Tanzania. One Touch Solutions ndio watakuwa wasemaji
wa msanii huyo.
Diamond kwa upande wake alisema anataka kufungua
ukurasa upya katika tasnia ya muziki nchini na kwa anaamini utasaidia katika
kumfanya aongeze nguvu zaidi katika kutunga na kutengeneza nyimbo zake.
“Hii yote ni kuhakikisha nafanya kazi zangu kwa
ufanisi badala ya kujirundikia mambo mengi, kuna watu walikuwa wakinitafuta
wanashindwa kunipata lakini sasa watakuwa wanafahamu ofisi ziko wapi na
wanawasiliana na menejimenti inawapa majibu, watu wa habari watakuwa na mtu wa
kuwasiliana nae moja kwa moja hata kama sipatikani,” amesema.
Diamond anatarajia kutoa wimbo wake mpya ambao
pia utarekodiwa na kampuni ya I-View. Tayari usaili umeshafanuyika kwa ajili ya
wale ambao wataonekana kwenye video hiyo.
I-View mbali na kazi kupiga picha, lakini pia
inatengeneza matangazo mbalimbali ya TV, Radio, mabango, ubunifu wa kazi
mbalimbali za sanaa.
0 Comments