KILA MMOJA ATAMBA KUIBUKA MSHINDI WA REDDS MISS TZ 2012

 Warembo wa Redds Miss Tz wakiwa katika hatua za awali kambini Giraffe Hotel wakiwa kwenye kupata chakula cha Mchana Oktoba 2 .2012
 
Warembo wa Redds Miss Tz wakiwa katika hatua mbalimbali za maelekezo katika kambi yao iliyopo kwenye Hotel ya Giraff hapa mmoja kati ya wafanyakazi wa Hotel hiyo bwana James Philbert akitoa maelekezo ya namna ya kutuma vifaa mbalimbali na ratiba ya chakula kwa kipindi chote watakapo kuwa kambini hapo.
Na Mwandishi Wetu

WASHIRIKI wa fainali za taifa za urembo mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2012' wametakiwa kuwa na nidhamu wakati wote watakapokuwa kambini wakijiandaa na shindano hilo litakalofanyika mapema mwezi ujao hapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na warembo hao jana baada ya kuwasili kambini, Mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, aliwaambia washiriki hao kuwa kila mmoja anawajibika kumuheshimu mwenzake na hakuna aliye na thamani kubwa kulimo mwingine.

Lundenga aliwaambia warembo hao wawe wanajitambua na hilo litawajenga katika maisha yao na kuwatakia waishi kwa furaha katika muda wote watakaokuwa kwenye kambi hiyo.
"Karibuni wote hapa kwenye hoteli hii ambayo itakuwa ndio makazi yenu katika kuelekea shindano la Redd's Miss Tanzania, ila wanaambia kwamba wote mko sawa na kikubwa ni kuwa na nidhamu," alisisitiza mratibu huyo.

Aliwaambia warembo hao kwamba wakiwa kwenye kambi hiyo watafundishwa mambo mbalimbali yanayohusiana na sanaa ya urembo, kujiandaa na maisha na kujitambua.

Aliwataja warembo hao waliongia kambini jana kuwa ni pamoja na Noela Michael, Magdalena Roy, Mary Chizi, Naombi Jones, Carren Elias, Venancy Edward, Warid Frank, Anande Raphaely, Lucy Stephano, Rose Lucas, Irene Veda, Joyce Baluhi, Virginia Mokiri, Fatma Twahil, Phina Revocatus, Belinda Mbogo, Lightness Michael, Elizabeth Diamond, Bridgitte Alfred, Diana Hussein na Irene David.

Aliwataja washiriki wengine kuwa ni Zuwena Nassib, Edda Sylivester, Flavia Maeda, Catherine Masumbigana, Jesca Haule, Eugene Fabian, Happiness Daniel, Happiness Rweyemamu na Babylove Kalalaa.

Mrembo anayeshikilia taji la mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's ni Salha Israel aliyetokea Kanda ya Ilala hapa jijini.


Post a Comment

0 Comments