Balozi Dr Diodorus Kamala akiwa Sir Andy Chande.
(Habari na picha kwa hisani ya Urban Pulse Creative)
Siku ya jumanne tarehe
25.9.12 Jumuiya ya Uingereza- Tanzania ( BRITAIN- TANZANIA SOCIETY) iliandaa
hafla fupi ya kusherekea miaka 50 ya Utaifa kati ya Nchi ya Uingereza na
Tanzania katika ukumbi wa The Royal Commonwealth Club, London. Wageni
mbalimbali pamoja na wanachama walijitokeza kwa wingi kuhudhuria hafla hii fupi
ilioandaliwa hususani kwa ajili ya kuchangia nchi ya Tanzania. Mojawapo ya
wageni waliohudhuria ni pamoja na balozi wetu Peter Kallaghe pamoja na mkewe
Mama balozi Joyce Kallaghe, Mwenyekiti wa Britain- Tanzania Society William
Fulton JP DL.
Mgeni rasmi katika
shughuli hii alikua ni Balozi wa Ubelgiji Mh Dr Diodorus Kamala aliyetoa mada
maalum kuhusu mafanikio, maendeleo na changamoto katika nchi ya Tanzania na
jumuiya nzima ya Afrika mashariki. Aidha Mh Dr Kamala alifafanua jinsi uchumi
wa Tanzania unavyokua kwa kasi kutokana na takwimu kutoka Benki ya Dunia pia
aliongelea kuhusu masuala ya utalii, mioundo mbinu, hali ya amani na usalama
ambazo zimepelekea wawekezaji wengi kuwekeza katika nchi ya Tanzania. Nchi ya
Uingereza ndio nchi pekee inayoongoza katika uwekezaji katika nchi ya Tanzania
Ikifuatiwa na India pamoja na Kenya
Pamoja na hayo Mh Dr
Kamala aliwashukuru wana jumuiya wa Uingereza- Tanzania kwa kuendelea kuisaidia
Tanzania kwa hali na mali ili kupambana na hali ya umaskini. Baada ya kutoa mada
yake kulikuwa na kipindi kifupi cha maswali na majibu kutoka kwa wanajumuiya
pamoja na wadau waliohudhuria.
Nae mwenyekiti wa
Computer 4 Afrika ndg Aseri katanga alitoa risala fupi ya kumshukuru mgeni
rasmi kwa kujitolea kwake kuja kujumuika na wanajumuiya pamoja na hotuba yake
nzuri kuhusu Tanzania.
Vile vile halfa hii
ilijumuisha uoneshwaji wa picha zilizochorwa na wachoraji kutoka Tanzania
ambazo zilinadiwa ili kuchangisha pesa za kuwasaidia kuwainua wadau wa tasnia
ya uchoraji Tanzania. Baadhi ya wachoraji ambazo picha zao zilionyeshwa ni
Mmadi Ausiy, Haji Chilonga, Hassan Kadudu, Florian Ludovick Kaija, James Haule
na Aggrey Mwasha.
Mama Balozi Joyce Kallaghe katika picha ya pamoja na Nelly Sheilamina na Elly mara baada ya mkutano.
Msanii Francia akiimba wimbo wa taifaWadau wakibadilishana mawazo
0 Comments