Wasanii wa kikundi cha Chemchem Arts maarufu kama Kidedea, wakiwa
jukwaani wakati wakionyesha mchezo wao uliokuwa na lelo la kuonyesha jinsi
sanaa za jukwaani zinavyoweza kufikisha ujumbe
Na Mwandishi Wetu
KIKUDI cha Chemchem
Arts Group, maarufu kwa jina la Kidedea kimelezea umuhimu kwa wasanii hapa
nchini kuandaa michezo ya kuigiza itakayokuwa na ujumbe mahsusi utakaoisadia
jamii ya Tanzania kutafakari juu ya muskabali wa masuala
mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.
Akitoa wasilisho
katika Jukwaa la Sanaa Katibu wa Kikundi hicho Christian Kauzeni amesema moja
kati ya mapungufu makubwa ya sanaa za hapa Tanzania ni kushindwa kufikisha
ujumbe utakaoifanya jamii kupata hisia, kuamka na kuchukua hatua juu ya masuala
mbalimbali yanayowakabili wanajamii.
Marta baada ya
wasilisho lake lililoeleza changamoto na mafanikio ya kikundi hicho katika
ufanyaji wa sanaa, kikundi hicho kilionyesha mchezo mfupi wa kuigiza uliojadili
pamoja na mambo mengine tabaka lililopo kati ya tajiri na masikini.
Mchezo huo ulionyesha
jinsi wananchi walivyo na hasira ya kuhukumu na kuwauwa vibaka na wezi wa
kuku huku wakiwaacha mafisadi wanaolihumu taifa wakiendela kutamba na magari ya
kifahari. Mchezo ulilenga katika kuwapa tafakari watazamaji juu ya namna ya
kuchukua hatua katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayojitokeza katika
maisha ya kila siku hapa nchini.
Wakichangia mara baada
ya wasilisho na mchezo huo, baadhi ya wadau wa masuala ya sanaa wameeleza
umuhimu wa jamii kuamka na kuchukua hatua stahili juu ya masuala muhimu badala
ya kuacha mambo makubwa kupita na kuisha kirahisi na badala yake wahoji kwa
kina kwa viongozi waliowachagua.
Akijibu hoja za
washiriki, Kauzeni alisema ni muhimu sana kwa watu kushiriki michakato
mbalimbali ya maamuziki ikiwa ni pamoja na kuhudhuria vikao vya serikali za
mitaa kwani huko ndiyo wananchi wanaweza kuanza kuleta mapunduzi ya kweli kwa
kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa.
0 Comments