Mashindano ya Redds
Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho
ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo
jumla ya 30 .
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim
Lundenga alisema mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na
mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na
ushindani wa hali ya Juu.
Washiriki wengi wa
mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo
Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta
hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.
Baada ya kukamilika
kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30
walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012
wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya
kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa Jijini
Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Tunapenda kuwajulisha
wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012
litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya
Blue Peal (Ubungo Plaza).
Kwa Upande wake Meneja
wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu
wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake
kwa wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo
wote waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo
mbalimbali.
Kwa kuzingatia
mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa Tanzania
atakuwa na muda mrefu wa maandalizi
kwani atatakiwa kuripoti katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia
katikati ya mwaka ujao. 2013.
0 Comments