MWENYEKITI WA UCHAGUZI ANGELO LUHALA
MAJINA ya vyama na wagombea watakaowania kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Vyama vya muziki nchini yanatarajiwa kutangazwa leo na Mwenyekiti wa uchaguzi huo Angelo Luhala.
Akizungumza leo asubuhi na Bongoweekend kwa njia ya simu Luhala alisema kwamba vyama vilivyojitokeza ni saba hivyo leo watatangaza majina ya waliokidhi vigezo katika uchaguzi huo.
Aidha Luhala aliongeza kwa kuvitaja vyama vinavyounda Shirikisho hilo kuwa ni Chama Cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA), Chama Cha Muziki wa Asili (TAFOMA),Chama Cha Muziki wa Taarab (TTA),Chama Cha Muziki wa Diski (TDMA), Mtandao wa wanamuziki MNET, Chama Cha Muziki wa Injili (CHAMUITA) na Chama Cha Muziki wa Mjini (TUMA) chama kimachowajumisha wanamuziki wa miondoko ya kufokafoka Rap, Hip Hop na Bongo Fleva.
Uchaguzi wa Shirikisho hilo unatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) uliopo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam .
Viongozi waasisi wa Shirikisho hilo ambao pia wanamaliza muda ni pamoja na Raisi Ibra Washokera, Makamu Che Mundugwao, Katibu Mkuu Salum Mwinyi,
wajumbe wa bodi ni Samuel Semkuruto, Seydou Mkandala, Rajab Samata.
0 Comments