Mbaraka Mwinshehe aliwahi kuimba akiisifia Morogoro na jinsi maji yanavyotiririka kutoka milimani.
Mwinshehe angekuwa hai pengine angefika maporomoko ya maji Endoro (Endoro Waterfalls) kushuhudia maajabu ya maporomoko hayo yaliyopambwa na msitu uliosheheni sauti za ndege na kupambwa na ulinzi wa Wanyamapori mbalimbali.
Mwinshehe angesema ama kweli Mungu anajua kuumba!!! haya ni maporomoko ya aina yake na hapa hupaswi kuwa na mtazamo wa wahenga kwamba Chema chajiuza na kibaya chajitembeza laah hashaa,
Maporomoko haya ya maji Endoro ni eneo zuri lililopo kusini ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro, takribani kilomita 6.5 kutoka mji wa Karatu.
Njia ya kuelekea maporomoko haya hupitia msitu na Mapango ya Tembo (Elephants Caves), na huchukua takribani saa 2–3 za matembezi ya wastani.
Mto Endoro hutiririsha maji mwaka mzima kutoka kwenye kingo za korongo, ukilishwa na chemchem za asili kutoka nyanda za juu za Ngorongoro, na kuanguka kwa urefu wa zaidi ya mita 40.
Hayo ni maporomoko ya maji ya Endoro ukifika huko utatamani uoge maji hayo na hasa ukiyavulia nguo.
Karibu Ngorongoro,
Maajabu yasiyoisha yanakuita.
Tumerithishwa, Tuwarithishe





0 Comments