MSHINDI TUZO ZA TASWA KUONDOKA NA KITITA CHA MIL.12.5


                                              Na Tasha Tryphone
MSHINDI wa jumla wa Tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka anatarajiwa kujinyakulia kitita cha Dola za Kimarekani elf 8 ambazo ni sawa na sh mil 12.5 za Kitanzania.

 Tuzo hizo zinazoaandaliwa na Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania(TASWA) zinatarajiwa kufanyika Juni 14 katika ukumbi wa Diamond Jublee(VIP A)jijini Dar es Salaam.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo hizo Imani Lwinga alisema wameaamua kutoa fedha taslimu tofauti na mwaka jana  walitoa gari ili mshindi afanye kile anachokihitaji.

 “Tumeaamua kutoa fedha taslimu na sio zawadi ya gari kama mwaka jana ili mwanamichezo ambaye ataibuka mshindi aweze kupata mwanga wa kuanzia maisha na kuja hiyo zawadi ataifanyia nini”alisema Lwinga.

Aidha Lwinga alisema anaimani kubwa Tuzo za mwaka huu zitakuwa bora zaidi ya mwaka jana kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya mpaka sasa.

Alisema mbali na zawadi hiyo ya jumla kila mshindi kila tuzo atajinyakulia Cheti, Kombe pamoja na sh mil 1 kila mmoja.

Nae Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto aliwashukuru SBL kwa sapoti kubwa ambayo wamewapatia ili kuweza kufanikisha zoezi hilo ambalo ufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuuthamini mchango mkubwa ambao wanamichezo mbalimbali wanautoa.

 Katika hatua nyingine Katibu Mkuu(TASWA)Amir Mhando aliitaja baadhi ya michezo mbalimbali ambayo itaingia katika kinyang’anyiro hicho kuwa ni, Riadha, Soka, Wavu,Netiboli, Kuogelea, Judo, Gofu, Tennes, Kikapu, Ngumi za kulipwa na ridhaa.
Mingine ni Baiskeli, Mikono, Olimpiki maalum pamoja na mchezaji bora wa ndani anayecheza nje na mchezaji bora wa nje anayecheza ndani pamoja na tuzo ya heshima ambayo mwaka jana milichukuliwa na Rais wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa.

Post a Comment

0 Comments