Pia jumuiya hiyo imesema katika taarifa yake hiyo kwamba, dini tukufu ya Kiislamu inaheshimu nyumba za ibada yakiwemo makanisa na mahekalu na hiyo JUMIKI inaamini kuwa matukio yaliyotokea kwenye manispaa ya Zanzibar tarehe 26 na 27 ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani Zanzibar, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya hiyo na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao lisifanikiwe.
Wakati huo huo kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar amesema kuwa, jeshi hilo litaendelea kuwasaka Viongozi wa Uamsho kwa gharama zozote zile.
Taarifa hiyo ya Kamishna Mussa Ali Mussa imekuja huku Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ikiwataka Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi na mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
0 Comments