MENEJA WA BENDI YA TWANGA MARTIN AFUNGUKA

                                                                MARTIN SOSPETER
BAADA ya kupata habari za kutimuliwa kwa Meneja wa bendi ya Twanga Bongoweekend iliamua kumpigia simu Sospeter ili kubalansi stori na yeye akawa na majibu haya kama ifuatavyo.
 Simu yake ambayo ilipipwa mara kadhaa ikawa iko busy lakini ukafika wakati ilisikika ikiita na kupokelewa Martin , ambapo alijibu maswali  kuwa anasemaje kuhusu kutimuliwa kwake katika bendi ya Twanga Pepeya naye bila kugwaya alijibu kwa kusema kuwa yeye binafsi hana habari zozote rasmi za kufukuzwa kwake katika bendi hiyo.
“ Sina habari yoyote rasmi ya kufukuzwa na hivi sasa dadangu tunavyoongea niko na wanamuziki wa Twanga tunatoka  Mbeya katika moja ya onesho lililofanyika huko ,hayo anayoyasema Mkurugenzi wangu mimi nimepata habari kutoka kwa wadau, marafiki zangu  waliopata habari hizo katika mitandao ya kijamii kama facebook na blogs mbalimbali ” alisema .
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa shutuma za kuwa anaihujumu bendi ya Twanga hazina ukweli wowote ,pia hajawahi kutoa ushawishi kwa wanamuziki hata mmoja kuihama Twanga  wanaohama wanahama kwa mapenzi yao na kufuata pesa.
"Kweli mimi nilifuatwa na uongozi wa bendi ya Mashujaa wakaniambia wananihitaji katika bendi yao mimi nikawambia kama wana sh. mil.20 pia  wanilipie nyumba kodi ya sh. 200,000 kila mwezi wakasema watanijibu au kama wakishindwa wanipe sh. mil.15 hilo ndiyo dau langu kwao lakini wamekaa kimya hadi sasa”.aliongeza Sospeter.

“Hivi kweli mimi ningekuwa na pesa ningekuwa nimechaa hivi? Laiti kama kweli Twanga kungekuwa na fedha au mimi nimepewa fedha ningebadilika hapa nilipo hata simu yangu ya kiganjani itakufa wakati wowote nayeye Mkurugenzi wangu Asha Baraka juzi alinikuta nikizikopi namba zangu za simu kwani wakati wowote inaweza kuzimika na isiwake tena sasa kama ningekuwa nina pesa si ningebadilika na kuwa na simu ya maana achilia mbali mbadiliko mengine” alisema.
Aidha alimalizia kwa kusema kuwa anaomba mungu afike salama akabiliane na hayo yaliyo mkuta kutokana na kuwa atakuwa hana kazi tena hapa mjini kutokana na kibarua chake  kuota mbawa.

Post a Comment

0 Comments