WAKATI tamasha maalum kwa vyombo vya habari ‘Media Day’ kwa mwaka 2012 likipangwa kufanyika Machi 24 kwenye ufukwe wa Msasani, Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imetoa shilingi mil.62.5 kwa ajiliya kudhamini tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria wa TBL Steven Kilindo alisema kuwa wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika biashara za kampuni yao.
Alisema kupitia udhamini wao fedha hizo zitatumika katika masuala mbalimbali hivyo watahakikisha linafanya kama ilivyokusudiwa kwani kama ilivyo lengo lake ni kuwakutanisha pamoja watu wa tasnia ya habari, kubadilishana mawazo na pia kupongezana.
“TBL itahakikisha bonanza la mwaka huu litafana na litakuwa la aina yake kuanzia katika michezo, burudani, vinywaji na vyakula, hivyo tunawaomba waandishi wajitokeze kwa kwingi ili kuweza kubiridika pamoja na kubadilishana mawazi,”Alisema Kilindo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) Juma Pinto pichani kulia ambayo ndiyo waandaaji wa bonanza hilo , pamoja na kuishukuru TBL kwa udhamini huo aliiomba kutoishia kudhamini kwenye mabonanza tu bali wafanye hivyo hata katika mafunzo mbalimbali yanayoaandaliwa na chama hicho.
“Tunaishukuru TBL kwa kutudhamini katika tamasha letu ambapo mmekuwa mkifanya hivyo kwa miaka kadhaa sasa, lakini tunaomba msiishie katika mabonanza tu kwani tuna semina ambazo tunaziaandaa mara kwa mara na zinahitaji kiasi kido tu cha fedha,”Alisema Pinto.
Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Taswa, Geoge John alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha waandishi 1500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali itakayotangazwa baadaye pamoja na burudani ya muziki
0 Comments