Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nurueli amesema kuwa, ana imani kubwa na wimbo wake mpya wa Mwanatanga ambao umeanza kutawala vituo mbalimbali vya redio na runinga unaweza kumrudisha katima chati za juu kimuziki.
Akizungumza na gazeti hili, msanii huyo aliyewika miaka michache iliyopita, amesema kuwa, wimbo huo ni sehemu tu ya albamu yake mpya ambayo hajaipa jina na kusifia kazi za Prodyuza Mike P The Spade aliyetengeza ngoma hiyo huku mtaalam wa video aitwaye Pete akionesha umahiri mkubwa katika video yake.
“Ni kazi f’lani ya ukweli nimeifanya pale studio za Don Lumak pande za Mwananyamala Mwinjuma ambayo imefanyiwa ubunifu mkubwa kwa mseto wa midundo ya mduara na kwaito na kuipa ladha safi isiyochosha kusikiliza au kucheza,” akatamba Nurueli.
0 Comments