Social Icons

Thursday, February 16, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) kila Jumatatu kuanzia saa 4 Asubuhi limekuwa likiendesha ‘Jukwaa la Sanaa’ kwenye ukumbi wake ulioko makao makuu ya Baraza Ilala Sharif Shamba.Katika jukwaa hilo linalohusisha wadau wote wa sanaa, hoja nzito na motomoto kuhusu tasnia ya Sanaa na Utamaduni zimekuwa zikijadiliwa na kujibiwa.

Katika Jukwaa la Sanaa Jumatatu ijayo ya Tarehe 20, Februari 2012, Kamati ya Vazi la Taifa itawapa fursa wasanii, wadau wa sanaa na wananchi kwa ujumla nafasi ya kufahamu hatua na mikakati iliyofikiwa katika mchakato mzima wa kupata vazi la taifa na kutoa maoni yao.

Wasanii na Wadau wa Sanaa na wananchi hawana budi kuja kwa wingi Kuanzia saa 4 Asubuhi kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba ili kupata fursa ya kukutana na Kamati ya Vazi la taifa
WOTE MNAKARIBISHWA
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI, BASATA
Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mtendaji
All correspondence to be addressed to The Executive Secretary
BASATA Arts Centre, Ilala Sharif Shamba, P.O. Box. 4779, Dar es Salaam, Tanzania.
Telephone: 2863748/2860485, Fax: 0255 - (022) - 286 0486 E-mail: info@basata.or.tz Website: basata.or.tz

No comments:

 
 
Blogger Templates