FFU! Ngoma Africa Band kuvamia Internationals African Festival Tübingen,Germany Mabakuli ya "Supu ya Mawe" uwanjani kila moja na lake! "FFU kwa hasira wamerusha song jipya "Supu ya Mawe" hewani "Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,kinatarajiwa kutumbuiza
jukwaani tena katika onyesho kubwa la aina yake African Internationals Festival,mjini Tübingen,ujerumani siku ya jumamosi 16.julai 2011. FFU hao wamziki pia wamepakua jikoni wimbo mpya uliobeba jina "SUPU YA MAWE" wimbi wenye ujumbe
mahusus kwa walimwengu ,ambao kwa sasa unasikia katika kambi ya FFU at www.ngoma-africa.com, wimbo huo utunzi wake kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na Christian Bakotessa aka Chris-B aka "Mshenzi" wa gitaa la solo.Wimbo huo "Supu ya Mawe" ujumbe uliomo katika wimbo huo unaonekana kuwa na nguvu na vitamin zote za maisha kuliko kikombe cha dawa.
kutokana na taarifa la gazeti moja la kimataifa hili http://www.africa-news.eu/entertainment/44-entertainment/2815-welcome-to-international-african-festival-in-tubingen-germany.html bendi hiyo maarufu inazidi kupata umaarufu na kujizolea washabiki kiani yake katika kila kona.
Usikose kuwasikiliza
at www.ngoma-africa.com hili nawe upate bakuli la "Supu ya Mawe"pichan ya kati afande Chris-B,aka "mshenzi " na mtutu wakepicha ya juu Kamanada wa FFU ras Makunja
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU AFUNGUA MRADI WA UIMARISHAJI NA
UHUISHAJI MAJI MKOROGO ZANZIBAR
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Ali Suleiman Ameir akikunjuwa Kitambaa
kushiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika hafla ya Ufunguzi wa Mradi wa
Uhuishaj...
4 hours ago
0 Comments