Amesema kuwa wataanza kupima maeneo yote ya serikali kwani hatua hiyo itasaidia kuwadhibiti wavamizi wa maeneo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kanosa iliyopo Kongowe Kibaha Mkoani Pwani Jordan Ngairo amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa uzio jambo linalochangia kuleta changamoto kwa waalimu na wanafunzi wakati wa masomo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas Mawazo akizungumza na wazazi, waalimu na wanafunzi katika mahafali hayo
Amesema kuwa wataanza kupima maeneo yote ya serikali kwani hatua hiyo itasaidia kuwadhibiti wavamizi wa maeneo huku amesisitiza kuwa zoezi hilo litakamilika mwakani.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji Africars Company Limited Hafidh Ameir Khamis amesema kuwa watoa madawati katika Shule hiyo pamona na samani za waalimu ikiwa ni katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan lengo ni kuboresha mazingira ya elimu.
Shule zingine ambazo ametembelea ni Misugusugu Sekondari ambako ameahidi kujenga ofisi za waalimu pamoja na uzio wa Shule huku kwa upande wa Shule ya Msingi Miisugusugu ambako alikua mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba ameelezwa kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu mkubwa wa matundu 12 ya vyoo na chumba kimoja cha Kompyuta (Computer Lab)
Makisio ya ujenzi na miundombinu hiyo kwa upande wa matundu 12 ya vyoo vya wanafunzi ni kiasi cha Mil.21,600,000 huku kwa upande wa chumba cha Kompyuta ni Mil.22 pamoja na Kompyuta kumi za kujifunzia.



0 Comments