WAZIRI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII PROFESA JUMANNE MAGHEMBE AAPA KUWAKAMATA WAUAJI WA WANYAMA PORI MB3LE YA WAHARIRI WA HABARI NCHINI TANZANIA

Mhariri wa The Guardian Limited Wallace Mauggo na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo Jesse Kwayu wakiwa kwenye  mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Veta , Mkoani Morogoro.
 Wahariri Imma Mbuguni na  Mike Tindwa  wakiwa kwenywe ukumbi wa mkutano
Mhariri wa gazeti la Nipashe Beatrice Bandawe kulia  na Khadija Kalili wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwendeshaji wa Blog ya Bongoweekend Khadija Kalili akijitambulisha.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Kebwe akikaribisha wageni ukumbini.
Aliyekuwa mgeni rasmi Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe , ambaye ameapa  kupambana na majingili wanaoua wanyama hasa Ndovu na Faru.Huku akizitaka nchi ambazo zinajishughulisha na biashara  hiyo kufunga masoko yao
Aidha katika kukuza Utalii wa nchi Maghembe alisema kuwa  serikali imepanga kujenga barabara sita ambazo zitatoka Mkoani Morogoro hadi Dar es Saalaam hivyo uchumi wa Mkoa wa Morogoro utapanuka zaid."

"Tutajenga bandari kavu , na kwa kuanzia tutajenga viwanda viwili mkoani  Morogoro jambo ambalo litachangia kukuza pato la uchumi wa nchi " Kutokana na ujenzi wa barabara sita ambazo pia zitapitisha garimoshi litakalokuwa likitumia umeme litarahisisha  hata makazi ya watu ambao tuna imani watakuwa wakiishi Morogoro na kufanya kazi Dar es Salaam huku wengine wakiishi Dar es Salaam lakini wakifanya kazi  Morogoro"alisema Maghembe.

Maghembe hakutaka kuwazungumza  majirani zetu ambao ni nchi ya Kenya kutokana na tabia zao za kuvuna kupitia vivutio vya kitalii na hifadhi za nchini."Kuhusu jirani zetu wa Kenya sitaki kusema lolote pia napingana na dhana iliyojengeka kuwa sisi hatujitangazi kimataifa huku akisema kwqmba lengo kubwa ni kuonfeza idadi kubwa ya watalii hasa ikizingatiwa Tanzania ni nchi ya pili ulimwenguni kwa ubora wa vivutio vya kitalii.

Profesa Maghembe alisema hayo leo wakati alipofungua mkutano mkuuwa wa mwaka wa TANAPA,unaofanyika  kwa siku tatu mkoani Morogoro.

Mkutano huo umehudhuriwa na Wahariri wa habari waandishi wa habari waandamizi pamoja na  wamiliki wa mitandano (Bloggers).

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Absalom Kibanda  akijitambulisha mbele ya Waziri Maghembe.
Mmiliki pia Mhariri wa gazeti la Jamhuri Deodatus Balile  akijitambulisha mbele ya Waziri Maghembe.
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akifafanua jambo kwenye mkutano huo.

Meneja Uhusiano TANAPA   Pascal Shetete akifafanua jambo

Post a Comment

0 Comments