HAKUNA MADHARA KENYA KUUTANGAZA MLIMA KILIMANJARO KUPITIA NDEGE ZAO:TANAPA




Mkurugenzi  wa Utalii  na Masoko TANAPA Ibrahim Mussa.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),wamesemahakuna madhara kwa Shirikala Ndege la Kenya kuweka nembo ya mlima Kilimanjaro kwenye ndege zake KQ, kwa sababu ni wanaleta watalii.

 Akizungumza leo kwenye Mkutano wa mwaka wa hifadhi za taifa Tanzania TANAPA, wa  mwaka   wa Hifadhi za taifa  Tanzania  na Wahariri  na  waaandishi waandamizi kutoka  vyombo  mbalimbali vya habari unaoendelea  kwenye ukumbi wa VETA ,Mkoani Morogoro Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Ibrahim Mussa alisema kuwa matangazo hayo ya bure ya mlima Kilimanjaro yamekuwa yakiwekwa kwenye ndege zingine alizozitaja na kuonesha picha ambazo ni Shirika la KLM na Shirika la ndege la Ethiopia.

 "Hakuna ubaya wowote kwa KQ kutangaza mlima Kilimanjaro, pia huwezi kuwa na haki miliki ya mlima kutokana na sheria za kimataifa, tunaweka nguvu sana kuilaumu kenya jambo ambalo siyo sahihi" alisema Mussa.

 Aidha aliongeza kwa kusema "tuseme ukweli ukiwa Amboseri nchini Kenya ni eneo la mbuga tu hivyo mlima Kilimanjaro unaonekana vuzuri zaidi hata ukipiga picha ndiyo maana wakenya husema 'Come Amboseri to see mount Kilimanjaro' wako sahihi alisema.

 "Tuwaache wafanye matangazo sababu wanatuletea fedha huku wao wakibeba hao watalii kupitia ndege zao" alisema Mussa. Akifafanua kuhusu kuyeyuka kwa barafu ya mlima Kilimanjaro alisema kuna utafiti mkubwa unaendelea na kufanywa na wataalam, pia akihusisha kuwa inawezekana ikawa ni mabadiliko ya tabianchi na pia huu ni mjadala mrefu linalohusu Sayansi zaid huku akiwatoa hofu watu kama mlima huo unaweza kuyeyuka.

Post a Comment

0 Comments