BODABODA WANANE KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA UHARIBIFU WA MALI

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Protas Mutayoba Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji ametoa taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa wnane ambao ni bodaboda katika Kijiji cha Kiwambo Kata ya Kitomondo Tarafa ya Kisiju Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani kwa tuhuma za kuharibu mali, ambapo wameharibu kwa kuvunja vioo vya mbele vya malori 16 na mabasi mawili ya kubeba abiria.

Tukio hilo limetokea Januari 16, 2026 wakati madereva wa bodaboda wakienda kumpumzisha bodaboda mwenzao katika Kijiji cha Kiwambo Wilayani Mkuranga ambaye inasadikika amefariki dunia baada ya kupata ajali ya kugongwa na gari maeneo ya Keko Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam.

Watu hao wamefanya matukio hayo kwenye magari waliyokuwa wanakutana nayo njiani kwa kuvunja vioo vya mbele kwa kurusha mawe na vipande vya tofali huku wakiwa wanakimbia kwa kutumia pikipiki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kamanda Mutayoba imeelwza kuwa Pikipiki tatu walizokuwa wanatumia watuhumiwa hao kama usafiri wao katika kutekeleza uhalifu huo zimekamatwa ambazo ni: MC 574 EQP, MC 496 FJG na nyingine yenye chassis No. BX2SWG66853G7 zote aina ya boxer.

Watuhumiwa hao wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mkuranga kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Post a Comment

0 Comments