Profesa Winiester Andersonkutoka( UDSM).
Watanzania na jamii nzima wametakiwa kujenga tabia ya kuwa watalii wa ndani ikiwa ni katika kukuza utalii na uchumi wa ndani. Endapo watanzania watawajengea watoto wao utamaduni wa kutangaza vivutio tulivyonavyo kwenye hifadhi za taifa, wanyama pori, maziwa , mapango , milima.
Hayo yamesemwa leo asubuhi na Profesa Winiester Anderson kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), kwenye mkutano wa mwaka wa hifadhi za taifa Tanzania na Wahariri na wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini unaendelea kwenye Ukumbi wa VETA mkoani Morogoro.
"Utalii wa ndani hasa barani Afrika unakua kwa kasi hivi sasa, na ina sadikika kuwa utalii wa ndani ni mara kumi zaidi ya watalii wanaotoka nje ya nje" alisema Profesa Anderson.
"Utalii wa ndani unakua zaidi ya asilimia kumi tofauti na ule wa kimataifa ambao unakua kwa asilimia tatu tu na ni wa msimu ambapo watalii wa nje ratiba yao ya utalii inafahamika huja nchini kati ya June na Oktoba kila mwaka, dunia nzima ndivyo ilivyo utalii wa kimataifa ukiwa chini unahitaji utalii wa ndani".
"Lengo la kutengeneza utalii wa ndani ni kuziba mapengo ya watalii na ukitangaza utalii wa ndani unabakisha fedha katika uchumi wa ndani ya nchi" alisema Profesa Andason Profesa.
Anderson ametoa wito kwa Watanzania kuanza kufundisha namna bora ya kumjali mteja, alisema hivyo kwa sababu hivi sasa changamoto ya watoaji huduma ni mbovu na wengi wao wanatakiwa kufundishwa thamani ya mteja ili kuweza kuongeza pato na kutoa sifa nzuri ya utalii ndani na nje ya nchi.
Utalii ni pato siyo idadi kubwa ya watalii tunawaambia watanzania wajiandae ili kuweza kukabiliana na changamoto ya kupqmbana na soko la utalii barani Afrika. Wakati huohuo amezungumzia umuhimu wa ukosefu wa taarifa kwa watalii kwani wengi wamekuwa waking'anywa taarifa za kibali za kununua vinyago ambavyo hunyang'anywa Uwanja wa Ndege na nchi kuonekana ni wezi.
"Inabidi itungwe sheria ambayo itaweka wazi haki ya mtalii kununua kinyago na haki yake ya kusafiri nacho tofauti na ilivyo hivi sasa kwani wengi bada ya kununua siku wanapoondoka huishia kulia baada ya kulazimika kuacha vinyago vyao hivyo inabidi hili jambo liangaliwe sababu halileti sifa nzuri kwa taifa letu" alisema Profesa Andason.
0 Comments