Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Picha na Geofrey Adroph(Pamoja Blog)
Picha na Geofrey Adroph(Pamoja Blog)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.
Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile, Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION
Meneja wa Biashara wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo
Munalove(kushoto) akimwelekeza mama mzazi wa Wema Sepetu jinsi ya kujiunga na WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mara bada ya kufanyika kwa uzinduzi huo
Msaniii wa Bongo Movie, Wema Sepetu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye baada ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari, katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini
Msanii wa Bongo Movie na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Maadam Wema Sepetu akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wake wa huduma ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION
Wema Sepetu akiwa amemkumbatia mama yake mzazi mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye
amesema kwamba serikali itakuwa pamoja na msanii nyota Wema Sepetu katika kila hatua ili kuhakikisha mwaba anapata haki zake bila kudhulumiwa.
Nnauye alisema hayo jana jioni kwenye uzinduzi wa mfumo wa kisasa kabisa wa msanii huyo nyota wa filamu nchini itakayofahamika ,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Wema almaarufu kama 'Maadam' alisema ya waandishi wa habari kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU
MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na
video mbalimbali yatakayowekwa kwenye
mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.
Wema Sepetu alisema kuwa huu ni mwanzo mzuri na aliahidi
kutumia huduma hiyo kutoa elimu kunufaisha jamii,kutangaza sanaa na utamaduni
wetu,kuwa karibu na wapenzi ama mashabiki wake wote watakaokuwa wanahitaji
kupata habari zake za kweli na uhakika.
Mfumo huu na wa kipekee kabisa kwa mwanadada huyo,umezinduliwa
na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi .
Mfumo huu ambao
utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote."Mfumo wangu huu ni wa
kipekee na wa kwanza katika Afrika Mashariki kwa msanii wa tasnia ya
Filamu,mfumo huu utaleta fursa nyingi sana zikiwemo ajira kwa vijana na wasanii
wenzangu na kutambulika kirahisi"alisema Wema Sepetu.
Kujua mafanikio na Umuhimu wa kazi za Usanii Tanzania,huduma
ya Wema Sepetu Mobile ni rahisi na ya uhakika,unatuma neno WEMA kwenda
15404 kwa makato ya sh. 60 tu na unaunganishwa na kuaanza kupokea taarifa na habari za Wema
sepetu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno,picha na video kutegemeana na aina ya
simu yako unayotumia.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye amempongeza Wema kwa kubuni mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote
na pia utamsaidia kumuingizia kipato na kuweza kuisaidia jamii inayomzunguka
kwa namna moja ama nyingine na kuahidi kuwa serikali itamsaidia ili kuhakikisha sasa anapata haki zake ambazo alizipoteza kuho nyuma.
"Inasikitisha tumeona vyombo vingi vya habari vikijinufaisha binafsi kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kutengeneza fedha nyingi huku Wema akiwa hana kitu sasa basi nimesimama hapa kwa niaba ya serikali naahidi haki yako haitapotea na utanufaika kutokana na jina lako wale ambao walikuwa wakitumia jina lako na kuandika mambo yasiyokuwa na ukweli mwisho wao umefika" alisema Nnauye
Wakati huohuo Meneja wa
Biashara wa Hartmann Trader ambao ndiyo
watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina aliweza kufafanua namna
huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujiunga na
kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo ambayo itapatikana kwenye simu za aina zote .
0 Comments