Wafanyakazi wa Benki ya Posta, wakiwa
kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada wa chakula katika kituo cha
Amazing step for Children foundation – Bagamoyo. Msaada huo una thamani ya
shilingi milioni 2.
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo.
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imetoa msaada ya mahitaji mbalimbali chakula, mavazi kwa kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu kiitwacho ‘Amazing Step for Children Foundation’ jana Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Kituo cha Amazing Step for Children Foundation kinahudumia watoto 43 na wazee wasiojiweza 6. Msaada huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 2, ulikabidhiwa na Afisa Mawasiliano ya Benki ya Posta, Chichi Banda.
Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Chichi Banda alisema waliamua kutoa msaada huo kwakuwa benki hiyo ni sehemu ya jamii, ina wajibu wa kuwa karibu nayo na kusaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali kila inapowezekana.
“Benki ya Posta inathamini sana watoto kwa kutambua kuwa wao ni viongozi wa kesho, pia jamii lazima itambue kwamba mtoto wa mwenzako ni wako, hivyo tuwatunze kwa upendo zaidi na kuwasaidia hasa wale wanaoishi kwenye mazingira magumu ili nao waweze kutimiza ndito zao”.
Alisema benki hiyo kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za kijamii kama kusaidia sekta ya elimu, afya na kufariji jamii katika vipindi vya majanga mbalimbali na pia kusaidia wale wasiojiweza na wanaohitaji msaada.

Naye Mkuu wa Kituo hicho, Daisy Ndege Sylvester aliushukuru Benki ya Posta kwa kuleta msaada huo katika kituo chake kwa ajili ya watoto na wazee. “Msaada huu umefika katika muda muafaka, tulikuwa na upungufu wa mahitaji muhimu mbali mbali katika kituo chetu kwa ajili ya watoto, hasa upande wa vifaa vya shule pamoja na chakula. Sasa tunaweza kuwahudumia watoto na wazee kwa idadi kubwa tofauti na mwanzoni katika Kituo hiki cha Amaizing, tunaomba wadau waendelee kujitokeza na kusaidia jamii inayowazunguka kama Benki ya Posta inavyofanya.
0 Comments