SERIKALI YAWAPA MOTISHA TIMU YA TWIGA STARS


Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni,Sanaa  na Michezo  jijini Dar es Salaam leo.

Na Frank Shija  WHUSM.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetimiza ahadi yake ya kuwapa motisha wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” kwa kuwapa kila mmoja shilingi Laki tatu taslimu kutokana na kufanikiwa kutikisa nyavu za Zimbabwe licha kutoibuka na ushindi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia James Wambura wakati wa mkutano wake na wachezaji hao leo jijini Dar es Salaam. 

Wambura alisema pamoja na Twiga Stars kufungwa kwa magoli 2-1 bado mmejitahidi sana katika ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwenye mashindano kama hayo walikuwa wanafungwa hadi magoli matano kwa sifuri.

Aliongeza kuwa kutokana na jitihada hizo anatimiza ahadi yake ya kumpatia kila mchezaji kiasi cha shilingi 300,000/= fedha ambazo anaamini zitawazidishia hari na morali ya ushindi katika mchezo wa marudiano.

“Kutoka na na jitihada zenu mlizozionyesha wakati wa mchezo huo ninatoa kwa kila mchezaji kiasi cha shilingi 300,000/= na ahadi hii inaendelea tena katika mchezo wa marudiiano” Alisema Naibu Waziri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) Amina Karuma alitoa wito kwa wachezaji kuhakikisha katika mechi ya marudio wanashinda kwa hari na mali ili kuonyesha thamani umuhimu wao.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuendelea kujitokeza kusaidia maendeleo ya michezo hasa Soka la wanawake kwani kumekuwa na changamoto ya wafadhili hali inayopelekea kusuasua. Motisha hiyo kwa wachezaji imetokana na michango ya wadau mbalimbali awalioguswa na timu hiyo wadau waliochangia mpaka sasa ni TCRA (10,000,000/=), ASAS(2,000,000/=), Mohamed Enterprises (2,000,000/=) na mdau ambaye akupenda jina lake litajwe (3,000,000/=) na kufanya mpaka sasa kuwa na jumla ya shilingi milioni 17.

Kwa wadau wanaopenda kuchangia watumie Akaunti namba 20110001677 Twiga Stars Special Fund NMB Bank House, kwa wale wanaotaka kuchangia vifaa waiwasilishe Wizarani mtaa wa Ohio Jengo la Golden Jubilee Ghorofa ya nane.

Post a Comment

0 Comments