VIFAA WANANCHI WA JIMBO LA RAHALEO


Wanafunzi wa Skuli ya msingi Rahale wakimpokea Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar alipowasili katika viwanja vya Skuli hiyo kukabidhi Vifaa viliotolewa na Mwakilishi wa Rahaleo kwa Wananchi wa jimbo hilo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Rahaleo kuhudhuria hafla ya kukabidhi Vifaa kulia Mwakilishi wa Rahaleo na kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Rahaleo Ndg Daudi Amani Bakari
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo na wanafunzi wa skuli hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Wanafunzi wa skuli ya msingi rahaleo wakimsikiliza Mhe Waziri Zainab akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa 

Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo wakifuatilia nasaha za Mhe Waziri Zainab wakati akizungumza na Wananchi wa jimbo la Rahaleo katika hafla ya kukabidhi vifaa,
         Wazee wa Kamati ya Jimbo la Rahaleo wakimsikiliza Waziri Zainab Omar akiwahutubia.
                                         Walimu wa Skuli ya Rahaleo wakifuatilia hafla hiyo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo,kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.


Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akimkabidhi Seti ya Vifaa vya ufundi gereji Kijana Zuberi Issa Ford,kwa ajili ya matumizi ya kazi zao za ufundi wa pikipiki  vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar,  akimkabidhi Vyerehani Mkuu wa Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Zanzibar Bi Hawa Seif Amour, kwa ajili ya matumizi ya Wanafunzi wa Kituo hicho,vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mkuu wa Chuo cha Ualimu Rahaleo Ndg Ussi Said Suleiman, kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi fedha Mkuu wa Chuo cha Ualimu Rahaleo Ndg Ussi Said Suleiman, kwa ajili ya kuogezea kusajili Chuo chao NACTE,fedha hizo ikiwa ahadi alioyowaahidi Viongozi wa Chuo hicho kwa ajili ya kufanya usajili wa Taifa.
Mzee wa kamati ya Jimbo la Rahaleo Ali Vuai Mussa akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wananchi wa jimbo la rahaleo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Zaiba Omar, na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kamati ya Jimbo la Rahaleo, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi vifaa. ilofanyika katika skuli ya rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Zaiba Omar, na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi vifaa. ilofanyika katika skuli ya rahaleo Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments