Mmoja wa wateja waliotembelea Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba akihudumiwa na Meneja Kiongozi Masoko na Ushirikiano wa, Bi. Eunice Chiume (wa kwanza kulia mbele).
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitoa huduma katika Banda lao kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba.
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakiwa katika Banda lao kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuwahudumia wateja wao.
Baadhi ya wateja kwenye banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia machapisho anuai ndani ya banda hilo
.
Baadhi ya wateja kwenye banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiangalia vipeperushi anuai ndani ya banda la NSSF.
WANACHAMA wote wa NSSF na wasio Wanachama Mnakaribishwa kujionea na kupata huduma mbalimbali zikiwemo, taarifa za jumla zinazohusu kujiandikisha uanachama, uwekezaji unaofanywa na Shirika, Maelezo kuhusu Bima ya afya itolewayo na NSSF,na kupata Kadi mpya.
Wageni wote wanaweza kujua kuhusu namna ya kuwasilisha maoni yao kupitia mfumo wetu mypa wa HaapyOrNot uliopo katika ofisi za Kinondoni, Ilala, Temeke na GDE- Waterfront Kwa kutumia mfumo huo mwanachama na asiye mwanachama anaweza kutuambia amefurahia huduma au Hapana pindi anapotembelea Ofisi za NSSF.
Pia wastaafu wote wanaofaidika na Pensheni za NSSF wataweza kupata pensheni kupitia mfumo mpya wa HIFADHI SMART ambapo mstaafu ataweza kupata fedha zake sehemu yoyote.
Vilevile wanachama na wasio wanachama mnakaribishwa ili muweze kujua kuhusu Huduma yetu mpya ya HIFADHI FASTA ambayo mwanachama sasa anaweza kulipa michango yake kupitia mtandao wa SELCOM wireless hivyo kumrahisishia yeye kuepuka usumbufu wa kutembea umbali mrefu ili aweze kuwasilisha michango yake.
0 Comments