Kutoka kushoto ni Mwanamuziki wa zamani wa miduara Omari Mkali , Hafsa Kazinja ( katikati) na Abdul Salvador.
IKIWA ni siku nne tu
tangu gwiji wa muziki wa dansi ambaye kwa sasa anaimba nyimbo za kumtukuta
mungu Cosmas Chidumule kutangaza mbele ya waandishi wa habari kutunga wimbo
maalumu wa kumuenzi Muhidin Gurumo sasa Malkia wa mmuziki katika miondoko ya Zouk Hafsa Kazinja
nayeye ametangaza kumwimbia mtafu huyo wa muziki wa dansi .
Kazinja ambaye kwa muda mrefu alikwa nje ya nchi nchini
Marekani anasema amepania kuibuka upya katika fani huku akiwa na ingizo lake la kwanza kati ya kumi aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu
wa NUTA Jazz Band uitwao ´Nimuokoe Nani´ anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.
Hafsa Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa
wimbo huo ili kumuenzi Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya
kufanya kazi hiyo kwa miaka 53 huku akiwa
na bendi mbalimbali nchini.
“Nimeamua kuimba wimbo huu wa ´Nimuokoe Nani ili
kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo
naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Kazinja aliyetamba na wimbo wake wa “Presha”
aliomshirikisha Banana Zorro.
Hafsa ameandaa wimbo huo wa Nimukoe nani” wimbo huo
amerekodi katika studio za Omari
Mkali inayofahamika kwa jina la OM Productions
iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam akisaidiana na mwanamuziki
nguli, Abdul Salvador .
“Nafurahi kwamba wimbo nimeimba wimbo baada ya kupata baraka zote kutoka kwa
mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe¨alisema Kazinja.
“Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya
kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya
kuridhika maana alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na
kuharibiwa ladha yake”, anasema kazinja, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake
zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.
Hafsa anasema katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na
kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa
wanamuziki nguli ndani na nje ya nchi wakiwemo Gurumo, Omar Mkali, Abdul Salvador na Lokassa
ya Mbongo wa Jmhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) aliyekutana na kufanya naye kazi alipokuwa ziarani nchini Marekani hivi karibuni.
Msanii huyu wa muziki
wa kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi ngoma hii ya kumuenzi Gurumo katika
tamasha la kumuenzi Gurumo lililopangwa kufanyika Oktoba mosi , 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es salaam.
“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye
tamasha hilo nami naahidi kuitendea haki ngoma ya gwiji huyo ya Nimuokoe nani hivyo
wadau wa muziki wasikose kuja kujionea
wenyewe jinsi siye wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa wetu wa
kazi, anaongezea Kazinja ambaye pia anaandaa video yake pamoja na ya ngoma zake
zingine mpya.
Mkongwe Abdul Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi
wa bendi ya Tancut Almasi iliyokua na maskani nyake mkoani Iringa iliyotamba na mtindo wake wa Fimbo
Lugoda , anamtaja Kazinja mmoja wa
wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti nzuri na kipaji cha hali ya juu hapa
nchini.
“Kwa kuweza kuimba wimbo wa Gurumo na kupatia kisawasawa inadhihirisha
kwamba Kzinja ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo kuimba nyimbo ya
wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Kazinja
“Hii inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na cha
zamani kufanya kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”,
anasema Salvador.
Omari Mkali, aliyetamba na bendi ya Chuchu Sounds, chini ya
marehemu Yusuf Chuchu, naye anamwelezea Kazinja kama moja ya majembe ya muziki
hapa nchini kwa upande wa kinamama, na kwamba anaweza kufika mbali endapo kama
moto aliokuja nao upya atauendeleza.
0 Comments