Kutoka kulia aliyekuwa mnenguaji nyota wa bendi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda na Mkurugenzi wake Asha Baraka katika ofisi za ASET, zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aisha Madinda akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa ASET , Kampuni inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka 'Iron Lady', Kiongozi wa bendi Luiza Mbutu, Kushoto kwa Aisha ni Haji Ramadhani 'Haji BSS' na Kalala Junior.
Aisha Madinda hivi sasa anajifua kwa mazoezi ya hali ya juu akijiwinda kurudi tena ulingoni ambako ameahidi kuwa atakuwa moto wa kuotea mbali , hiyo ni baada ya kutopea katika utumiaji wa dawa za kulevya ambazo hivi sasa amefanikiwa kuacha na kuwa akipata huduma katika kliniki ya watumiaji wa dawa hizo iliyopo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na Bongoweekend katika nyakati tofauti wasanii wenzake kama Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu 'Mamaa Brian' alisema kwamba wanashukuru mungu kwa kuona msanii mwenzao ameweza kupambana na utumiaji wa dawa za kulevya na wanamkaribisha kwa mikono miwili kundini. Wakati huohuo Kalala Junior alisema kwamba "Kama nilivyotunga wimbo wangu wa Nyumbani ni Nyumbani' nasema Kurudi nyumbani siyo kosa hivyo jamii na wadau wampokee Aisha kwa mikono miwili.
Diplomasia ya Mhe.Rais Samia Inawaleta Wakuu wa Nchi za Afrika Kushiriki
Mkutano wa M300 -Dkt.BITEKO. * Asema mafanikio ya Sekta ya Nishati nayo
imeibeba Tanzania Mkutano wa M300 * Vijiji vyote Tanzania vyafikishiwa
umeme * Ataja faida za Mkutano wa M300 Nchini
-
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (kulia) pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson
Msigw...
1 hour ago
0 Comments