MWENYEKITI
WA MADEREVA BARABARA YA PASUA-STENDI JOSEPH LUMWE
KATIBU
WA WASAFIRISHAJI (WAHIPA) SEKI MSHANA
JUMA
SAID MMOJAWAPO WA MADEREVA
OCS
BRUNO AKIWASILI ENEO LA TUKIO
OCS
BRUNO AKIZUNGUMZA JAMBO
Dereva aliyejitambulisha kwa jina la Juma Said amesema tangu barabara ya Pasua ianze kufanyiwa marekebisho na Manispaa ya Moshi Polisi hao wameongeza nguvu ya kuja kuyakamata magari yao na kuyaacha yale ya Kwa Mtei na Kahe.
Said ameongeza kusema gari halikosi kosa hata kama ni jipya na Polisi hao wamekuwa wakitumia njia hiyo kujipatia fedha kutoka kwa madereva na wakati mwingine wafikishwapo Kituo cha Polisi wamekuwa wakipewa makosa tofauti na walivyokuta.
Pia Madereva hao wamesema kumekuwa na baadhi Polisi wa Usalamawakati wakitaka kuwakamata hutumia magari ya Polisi kwa kuyaweka uso kwa uso badala ya kusimamisha kwanza ndipo waendelee na mahojiano kitu ambacho wamekiita ni maonevu ya hali ya juu.
Wamiliki na Madereva hao wameapa kuwa kama masuala yao yasipopewa ufumbuzi wa kina wataendelea kufanya mgomo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madereva wa Magari ya Pasua-Stendi Kuu Joseph Lumwe amekiri kuwepo kwa mgomo huo amabao ameuita kuwa ni chachu kwa madereva wa magari mengine ya abiria mjini Moshi wanaonewa na Polisi wa Usalama barabarani.
Lumwe amesema Polisi wamekuwa na uonevu wa hali ya juu kwa safari zao huku wakijua kuwa ustarabu wakati mwingine ni mzuri kutokana na ukweli kwamba barabara ya Pasua sio nzuri sana hivyo gari kuchakaa ni rahisi sana kuliko gari ambalo safari zake ni lami mwanzo mwisho.
Hata hivyo Katibu wa Usafirishaji (WAHIPA) Seki Mshana amesema Polisi Kitengo cha Usalama barabarani wanapaswa kuwasikiliza na kuwachukulia hatua madereva na Polisi wanaokiuka taratibu za uendeshaji.
Seki amekiri kuwepo kwa madereva watovu wa nidhamu katika barabara hiyo lakini kubwa linalotakiwa kufanyika ni kuwachukulia hatua kama madereva na sio kama gari kwani wakati mwingine huweza kukutwa akiwa amelewa na anaendesha chombo cha moto na abiria ndani.
Pia kwa Polisi Uslama barabarani wanaotumia ubabe katika kazi yao ni mbaya kwani imewafanya wawone kuwa ni adui zao hata kuitisha mgomo.
Aidha OCS Bruno kwa upande wake amewataka madereva hao kuendelea na shughuli kama kawaida, na kwamba kero zao amezipokea na kuahidi kuzifanyia kazi likiwemo la maafande wanaotumia ubabe badala ya kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Hadi tunakuletea habari hii, tayari mgomo ulikuwa umemalizika na usafiri wa Pasua-Stendi ukiendela kama kawaida baada ya OCS Bruno kufika katika sehemu walipofanyia mgomo katika soko la Manyema Mjini Moshi mapema leo, na kutafuta suluhisho la haraka.
0 Comments