MGOMBEA SAID MOHAMED ANAYEGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA LIGI AONDOLEWA PINGAMIZI



Wakati mchakato wa uchaguzi ndani ya shirikisho la soka nchini TFF na bodi ya ligi kuu ukizidi kupamba moto huku baadhi ya wagombea wakiwekewa mapingamiz na wadau mbalimbali wa soka nchi hatimaye pingamizi alilowekewa mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Said Mohamed limeondolewa.

Pingamizi liliwekwa kwa mgombea huyo lilitoka kwa katibu wa zamani wa chama cha soka mkoa wa kisoka wa Kinondoni Frank Mchaki ambaye aliweka pingamizi hilo kutokana na kwamba mgombea huyo hakuwa kiongozi wa klabu yoyote nchini.

Hata hivyo kufuatia kamati ya uchaguzi kukutana na wagombea na wawekaji wa mapingamizi hayo kwa lengo la kufanyika mapitio ya mapingamizi mbalimbali na sababu za mapingamizi hayo imedhihika kuwa Mzee Said Mohamed ni kiongozi wa Azam fc kwa nafasi ya mwenyekiti.

Akiongea na waandhishi wa habari hii mwekaji wa pingamizi hilo Mchaki amesema ameridhishwa na zoezi la kuhakiki nafasi ya uongozi ya mzee Said Mohamed ndani ya Azam kwani aliweka pingamizi kwa kuwa alikuwa hana uhakika kama Said Mohamed ni kiongozi wa kuchaguliwa wa Azam licha ya kwamba amekuwa akisikia kuwa ni kiongozi wa klabu hiyo.

Mchaki amesema mzee Said Mohamed alikuja na vielelezo kamili ambavyo vimeonyesha kuwa alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti 1/10/2012 alikuwa ni mwenyekiti wa Azam.

Kumbuka moja ya sifa ya kuwania nafasi ya uongozi ndani ya bodi ya ligi, mgombea anapaswa kuwa kiongozi katika moja ya vilabu vya ligi kuu.

Post a Comment

0 Comments