MC DONALD TRAINING CENTRE WATOA ELIMU YA LIVELINE KWA WAKANDARASI WA UMEME

 MHANDISI Donald Mwakamele MC Donald , ambaye ni mmiliki wa Chuo Cha MC Donald Live Line Technology , akibadilisha vikombe  vya umeme  katika eneo la chuo hicho kilichopo Mvomero, Morogoro kwa kutumia teknolojia hiyo ya kufanya matengenezo ya umeme bila kuzima njia ya  umeme  wakati matengeneo yakiendelea.
 Hapa akijitayarisha kabla ya kupanda katika nguzo ya umeme na kunesha teknolojia ya LiveLine.
 SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeingia lawamani baada ya kukata umeme kwa madai ya kumzuia Mhandisi wa Chuo kipya cha Teknolojia ya Liveline Donald Mwakamwele asifanye shughuli zake chuoni hapo katika ziara maalum iliyofanyika Septemba 13 Mvomero, Morogoro.
Akiwa na ugeni wa wahandisi kutoka nchi 18 kati ya 26 kutoka Afrika   ambao walifika katika Chuo Cha Mc Donald Liveline Training Centre , kilicho chini ya uongozi na mmiliki Mhandisi Mwakamele .
Wahandisi hao walifika  katika chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara ya maalumu ya kujifunza teknolijia hiyo kwa vitendo  jinsi ukarabati wa umeme unavyoweza kuendelea bila ya kuzima Umeme kitendo cha kuzima umeme kwa dadika 10 tu husababisha hasara kubwa kwa taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari waliokuwemo katika ziara hiyo, mhandisi huyo alilaani kitendo  cha kunyimwa kibali na kukatiwa umeme ambacho amekiita ni cha hujuma  zilizofanywa na watendaji wa TANESCO wenye nia ya kumkwamisha katika majukumu yake bila kujali ugeni alioongozana nao na umuhimu wake kwa taifa pia.
“Nalaani kitendo cha TANESCO kuninyima kibali na kukata umeme kwa madai kwamba eti wanafanya ukarabati huku wakitambua kwamba mimi ni mtaalamu wa Liveline ambapo matengenezo yanaweza kuendelea bila kukata umeme, hii yote ni kutaka wanikwamishe nisiwaonyeshe wageni namna Liveline ilivyo muhimu na inavyofanya kazi bila kukata umeme”.
“Ni fedheha kwa uongozi wa TANESCO Morogoro kunihujumu na kuwakosesha wananchi wenye kiu ya maendeleo… teknolojia hii imefanyakazi kwa miaka 20 iliyopita hapa nchini,” alisema mhandisi Mwakamele.
Awali alilishangaa shirika hilo kuikataa teknolojia hii ambayo ilitambulishwa mwaka 1988 na kufanyakazi kwa ufanisi huku akisisitiza kwamba teknolojia hiyo inauwezo wa kufanya matengenezo ya umeme bila kuathiri huduma hiyo kwa wananchi.
Aidha ametoa ofa kwa wakandarasi wa TANESCO kujifunza bure teknolojia ya Liveline na kusema ni mpango wa chuo hicho kufungua matawi mikoani.
Wahandisi hao kutoka nchi za Malawi, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na kwingineko wameupongeza uwekezaji wa teknolojia hiyo waliodai umewavutia kwa vile inatoa chachu ya maendeleo barani Afrika.
Kabla ya ziara hiyo Wahandisi hao  walikuwa wakihudhuria  mkutano mkubwa  wa sekta ya Umeme  Afrika Mashariki (EAPIC), uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuwatanisha watendani wakuu wa makampuni  26  kutoka nchi  mbalimbali  zinazohusisha  na nishati ya  umeme  katika bara la Afrika.
Lakini licha ya TANESCO kukata umeme  waliweza kuoneshwa  namla teknolojia ya Live Line inavyofanya kazi  na kuliwezesha Shirika hilo kuweza kuokoa  kiasi kikubwa cha fedha  kwani kwa kukata umeme  wakati wa matengenezo  huleta hasara kubwa  kwa nchi na mzigo kwa wananchi kwa ujum.a. Chuo Cha MC Donald kipo maeneo ya Mvomero, Morogoro natarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni
 




 Baadhi ya Wahandisi wakiwa katika picha ya pamoja  na mmiliki wa chuo cha ugavi cha  Mc Donald.
 Wahandisi wakiendelea na ziara sambamba na kukagua majengo ya chuo cha Mc Donald.
  Mhandisi na Mkurugenzi wa Chuo Donald Mwakamele Mc Donald katikati .
 Meneja Biashara wa MC Donald  Garry Craig  akifuatiwa na baadhi ya  wahandisi.
 Waandishi wa Habari kuitoka vyombo mbalimbali wakiwa katika ziara hiyo.
 Mkurugennzi Mtendaji pia mmiliki wa  chuo cha MC Donald na Meneja wa Biashara Garry wakiteta.
 Sehemu ya wahandisi wakipata maeleo kutoka kwa MC Donald jinsi  teknolojia ya Live Line.
  MC Donald akiendelea kutoa maelezo.
 Ikafika zamu ya Mhandisi Garry kutoa maelezo.

Post a Comment

0 Comments