NMB YAENDESHA DROO YA KWANZA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB

Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa akifafanua jambo wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya Jenga Maisha Yako na NMB iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mineja Bidhaa wa Selcom Wireless, Julio Batalia na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Elimsu.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Baada ya ubinafsishaji wa benki ya NMB mwaka 2005, NMB iliendelea kukuza mtandao wake wamatawi, ndani ya miaka mitano matawi yameongezeka kutoka 100 hadi matawi zaidi ya 140. Idadi ya watejawa NMB imekua kutoka wateja 600,000 mpaka wateja1,600,000 hiyo ni asilimia 30 au 40 ya watanzania wote ambao wana akaunti katika benki zote za Tanzania ili kurahisisha na kuboresha utoaji huduma. NMB ilianza kutoa huduma ya ATM kutoka wateja 0 mpaka wateja milioni moja na laki sita na pia namba za mashine za kutolea fedha (ATM) zimekuwa kutoka 0 mpaka 450 na pia NMB ndio benki ya kwanza Tanzania kuanzisha huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi, NMB Mobile. Hadi sasa kuna wateja 600,000 wanaotumia huduma ya NMB Mobile
NMB imeendelea kubuni na kuanzisha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wateja wake. NMB ndio benki pekee Tanzania yenye akaunti kuanzia za watoto wadogo, wanafunzi, wafanyakazi, wakulima na wastaafu. Pia NMB imeendelea kuboresha faida wateja wanazozipata kutokana na kuwa na akaunti NMB. Hivi sasa mteja wa NMB ana chaguo pana la njia za kupata huduma anaweza kupata huduma ndani ya benki, kutumia ATM, kutumia NMB mobile au huduma ya Intaneti.
NMB ni benki inayowajali sana wateja wake hata wakati washida, mwaka jana, 2011 NMB ilizindua huduma ya NMB Faraja inayomwezesha mteja wa NMB Personal Account kupata mkono wa pole kati ya shilingi 600,000 hadi 1,200,000. Hadi sasa, huduma ya NMB Faraja imewanufaisha wateja wengi wa NMB, nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments