(Picha na Mpiga Picha wetu)
WAKATI bendi ya African Stars (Twanga Pepeta)itapamba shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Sinza 2012 lillopangwakufanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Mawela Social (Ten Star Lounge) uliopo karibuna hotel ya Vatican City, Kamati ya Miss Tanzania leo itatembelea warembo hao kwa lengo la ‘kuwafunda’ tayari kupanda jukwaani.
Mratibu wa kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary alisema jana kuwa Twanga Pepetaimeandaa zawadi kwa mashabiki wake na wale wa urembo kwa kuwapa uhondo wanyimbo mbili mpya ambazo zitakuwa zinasikika kwa mara ya kwanza jukwaani.
Nyimbo hizo ni Mapambano ya Maslahi uliotungwa naMuumin Mwinjuma, Shamba la Twanga ambao umetungwa na Greyson Semsekwa na mmojaambao haujapewa jina uliotungwa na Jumanne Saidi ambaye amfunga ndoa namnenguaji wa bendi hiyo, Asha Sharapova.
Alisema kuwa nyimbo hizo ni zawadi kwa mashabiki waTwanga wa Sinza na vitongoji vyake kwani bendi hiyo haijafanya shoo huko muda mrefu.
“Tunatarajia kuwa na shoo nzuri kutoka kwa warembona bendi ya Twanga Pepeta ambayo mwaka huu imeshinda tuzo mbili katika tuzo zamuziki Tanzania,” alisema.
Kuhusiana na ziara ya Kampuni ya Lino InternationalAgency, Majuto alisema kuwa Lundenga na wenzake watafanya mazungumzo na warembohao baada ya mazoezi yao ya pamoja.
Alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya faraja kwawarembo na kamati ya Miss Sinza kutokana na ukweli kuwa ujio wao ni wa Baraka nahitimisho la mashindano ya vitongoji nchini.
“Miss Sinza ndiyo inafunga pazia la mashindano yaVitongoji (vituo) nchini, Lundenga na wenzake wanakuja kutoa baraka zao kablaya kuanza pilikapilika za Redds Miss Tanzania,” alisema.
Shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold,Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com,Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.
0 Comments