Katibu Mkuu wa BASATA Ghonje Marego akiwa katika picha ya pamoja na Rais mpya wa Shirikisho la Muziki pamoja na wajumbe waliochaguliwa.
Mwanamuziki mkongwe Mafumu Bilali 'Bombenga' akiwa katika chumba kilichofanyika uchaguzi wa Shirikisho hilo mwishoni wma wiki.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA)
SHIRIKISHO la muziki nchini wamefanya uchaguzi mkuu chini ya Baraza la sanaa la Taifa (BASATA), na kufanikiwa kumpata Rais wa chama hicho, Ado November kutoka Chama Cha Muziki wa Injili nchini (CHAMUITA).
Katika uchaguzi huo Ado alichuna na wagombe wengine watatu walio kuwa wakiwania kiti cha Urais wa shirikisho hilo ambao ni Abdul Salvador (CHAMUDATA), Frederick Mariki (TUMA) na Samuel Semkuruto (TDMA) .
Katika nafasi za wajumbe wa chama hicho ni Maumbile Ali Msanda, Rajab Samata, Ency Mulusaka, Doris, Che Mundugwao, Samuel Semkuruto na Samwel Mbwana ambao walipita kwa kuchaguliwa.
Akizungumza wakati wa uchaguzi Katibu mkuu wa BASATA, Ghonje Materego aliwataka viongozi hao wafanye kazi kwa ushirikiano na upendo ili kuleta mafanikio katika chama hicho.
Naye November aliwashukuru wajumbe wa uchaguzi huo kwa kumpigia kura na kuahidi kufanya nao kazi bega kwa bega pamoja na kukiletea chama hicho mafanikio ikiwa ni pamoja na kukitangaza kimataifa.
0 Comments