Fred Mariki 'Mkoloni'
WAGOMBEA wanne amejitokeza kuwania kiti cha urais cha Shirikisho hilo ambao ni Abdul Salvador Chama Cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), Ado November Mwasongwe Chama Cha Muziki wa Injili (CHAMUITA), Frederick Marick Chama Cha Muziki wa Mjini (TUMA) na Samuael Semkuruto anayewania kwa tiketi ya Chama Cha Muziki wa Diski (TDMA).
Wanaogombea nafasi za ujumbe Maumbile Ali Msanda na Rajab Samata na Ency Ntepa Mulusaka wote (CHAMUDATA), Doris Kabanga na Che Mundugwao (TAFOMA) .
Wengine ni Samuel Semkuruto (TDMA), Ado November Mwasongwe (CHAMUITA)
Uchaguzi huo utafanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kuanzia saa tatu uliopo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Aidha Luhala aliongeza kwa kusema kuwa yapo majina ya wagombea kadhaa ambayo hayakupitishwa kutokana na kutokidhi vigezo hasa vya elimu.
Viongozi waasisi wa Shirikisho hilo ambao pia wanamaliza muda ni pamoja na aliyekuwa Raisi Ibra Washokera, Makamu Che Mundugwao, Katibu Mkuu Salum Mwinyi, wajumbe wa bodi ni Samuel Semkuruto, Seydou Mkandala, Rajab Samata.
Kwa mujibu wa Luhala kutokana na mabadiliko ya katiba hakutakuwa na Makamu wa Shirikisho kama ilivyokuwa katika katiba yao ya awali ambayo hivi sasa imefanyiwa mabadiliko na kuondoa baadhi ya nyadhifa.
0 Comments