Elizabeth Michael Lulu akitoa tabasamu Mahakamani leo.
KESI ya mwigizaji kinda Elizabeth Michael 'Lulu' jana ilipigwa kalenda hadi itakapotolewa uamuzi wake .
Lulu akiwa chini ya ulinzi wa maaskari magereza wanawake ambao walikuwa sita na wanaume saba hawapo pichani.
Hiyo ni kwa mujibu wa Jaji Dk. Fauz Twaib aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo iliyofikishwa Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam kwa shauri la ufafanuzi juu ya umri wa mshtakiwa.
Jaji Twaib huyo alidai Mahakamani hapo kuwa kutokana na utetezi kuwa mrefu hivyo hana budi wa kupata muda ili aweze kuupitia na uamuzi wake utatolewa Juni 11 katika Mahakamani hiyo.
Aidha mawakili wane ambao wanamtetea Lulu wameiomba Mahakama hiyo kuchunguza umri wa Lulu au watoa idhini kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuchunguza.
Mawakili wa mtuhumiwa Lulu maombi waliyoyaleta katika Mahakama Kuu ni mapya na vifungu walivyotumia haivipi mamlaka kwa sababu ya maombi mapya, walitakiwa kukata Rufaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walitakiwa.
Mawakili waliokuwa upande wa Serikali ni Shadrack Kimaro na Elizabeth Kaganda huku mawakili wanne ambao wanamtetea Lulu ni wane ambao ni Jacqueline Dimelo,Kennedy Fungamtama, Fulgency Massawe na Maico Kibatala.
Hata hivyo hali ilikuwa ya utulivu tofauti na ilivyozoeleka mwanzoni mwa kesi hiyo ilivyoanza kusikilizwa pia mtuhumiwa nayeye alikuwa katika hali ya kawaida na kuwa na sura yenye tabasamu na kuweza kupeana ishara ya salamu na baba yake mzazi aliyefika Mahakamani hapo kusiliza kesi kesi ya binti yake.
Mara kwa mara Lulu alikuwa akipepesa macho kila kona ya ndani ya Mahakama hiyo na hata kuwaangalia watu wachache waliokuwemo ndani ya Mahakama.
Jopo la Mawakili walichukua muda mrefu katika kubishana masuala mbalimbali ya kisheria.
Lulu anakabiliwa na tuhuma za kusababisha kifo cha aliyekuwa mcheza filamu nyota nchini Steven Charles Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake Sinza Vatican Jijini Dar es Salaam.
0 Comments