TAMASHA LA MAKABILA MIKOA YA ARUSHA KILIMANJARO KUFANYIKA SHEIKH AMRI ABEID


TAASISI ya Maendeleo ya Uswisi imetoa udhamini katika kufanukisha tamasha la utamaduni la kwa mikoa ya Kanda Kaskskazini litakaofanyika kwa siku mbili.

Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Ofisa Utawala na Habari Ismail Mnike alisema kwamba tamasha hilo limepangwa kufanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Alisema lengo la tamasha hilo ni kusaidia kudumisha amani na kusamehea mbambo mbalimbali yaliyojitokeza katika siasa kwa wagombea waliotofautiana katika chaguzi mbalimbali huko nyuma.“Kwa mfano ugomvi wa kugombea aridhi kwa wakulima na wafugaji hapa ndiyo huwa sehemu ya kupata muafaka kwa viongozi wa kiserikali na kimila husaidia kufanya upatanisho” alisema Mnikite.

Aliongeza kwa kusema kuwa kwa kupitia tamasha hilo itakuwa ni njia mojawapo katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo mkoani Arusha kama mlima Kilimanjaro na Ngorongoro.Katika tamasha hilo mbali ya kuwahusisha wasanii wa ngoma za asili ikiwemo makabila makubwa yaliyomo mkoani humo pia wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva watakuwepo tamasha hilo limepangwa kufanyika Novemba 11 hadi 12 mwaka huu.

“Tamasha hili litafanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni litakuwa ni la bure , mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi”.Alivitaja vikundi vitano vya ngoma za asili kutoka makabila ya Wamaasai, Wachagga, Wapare, Wamang’ati na Wambulu yatashiriki katika tamasha hilo.

Na kwa upande wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakaokuwepo ni Afande Seel, Mandoji & Domo Kaya, Godzilla, Adam Mchomvu na wengineo.Wadhamini wa tamasha hili ni Kalunde General Supplies, Clouds FM, Endeleza Foundation, Channel Ten, Magic FM, Ultimate Security, Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC).

Post a Comment

0 Comments