SIMBA YANGA WAPEWA HUNDI ZAO NA TBL ZENYE THAMANI YA SH.MIL4O

Viongozi wa Simba na Yanga mara baada ya kupokea mfano wa hundi zao kutoka TBL.


Picha /Habari na Francis Dande.
Wadhamini wakuu wa vilabu vya Simba na Yanga kampuni ya bia Tanzania (TBL)
Kupitia bia yake Kilimanjaro Premium Lager jana ilikabidhi hundi zenye thamani ya sh Milioni 40 kwa vilabu hivyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkataba wake.
Yanga ambao ndio mabingwa wa msimu uliomalizka wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilipata kitita cha sh. milioni na Simba iliyoshika nafasi ya pili ilipata hundi yenye thamani y ash milioni 15.
Akiongea katika ofisi za TBL jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, David Minja alisema kuwa ‘baada ya kumalizika kwa msimu wa 2010/2011 wa ligi ya soka nchini, sasa wakati wa kutimiza ahadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili wa ligi Kuu.
‘TBL ingependa kutoa shukrani za dhati kwa Chama cha mchezo wa Soka nchini TFF, timu zote zilizoshiriki pamoja na viongozi na wanachama wao kwa ushirikiano wa hali ya juu waliouonyesha tangu kuanza kwa ligi mpaka mwisho wa msimu’.
Aidha Minja alisema kuwa TBL itaendelea kuwa mdhamini wa vilabu hivi vikongwe vyenye mashabiki wengi zaidi hapa nchini na kuwapa motisha wachezaji na viongozi ili waweze kujituma zaidi na kushinda vikombe na kuipa heshima nchi yetu katika ngazi za kimataifa.
Katika msimu uliopita wa ligi wa 2009/2010, timu ya Simba iliibuka bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kujinyakulia kitita cha sh milioni 25 kutoka TBL na timu ya Yanga Yanga ilishika nafasi ya pili ikajinyakulia kitita cha sh. milioni 15.
Viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga walihudhulia makabidhiano hayo ya hundi hizo kwa upande wa Simba makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kabulu’ alisema kuwa fedha hizo zitasaidia katika kuchangia maendeleo ya klabu hiyo inayojiwinda na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhindi ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kongo.
Katibu Mkuu wa Yanga,Mwesingwa Selestine alisema kuwa udhamini wa kampuni hiyo umekuwa chachu ya kufanya vizuri katika Ligi na hatimaye kuwa mabingwa kwa msimu uliomalizika, aliitaka kampuni hiyo kuongeza udhamini wake ili vilabu vingine ili kuleta msisimko na ushindani wa kweli katika ligi.

Post a Comment

0 Comments