ZOGO LA BABA WA KAMBO SASA KUENDELA JUNI 26 UJERUMANI



FFU wa Ngoma Africa band jukwaani Heidelberg City,25-06-2011 Pia 26.06.2011 Live ndani ya Africa Tage festival,Freudenstadt, Ujerumani Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" almaarufu FFU,imejikuta katika mshike mshike usio na mwisho uko nchini ujerumani..kwani bendi hiyoinaparamia jukwaa la AFRIKA DAYS Festival siku ya jumamosi 25.06.2011 kuanzia saa 3 usikukatika mji wa Heidelberg,Ujerumani, ambako washabiki wa miji ya Heidelberg,Mennheim,n.k watajirushana gwaride la mziki wa FFU ndani ya ukumbi Karlstorbahnhof,mjini Heidelberg. Jumapili ya 26.06.2011 Kikosi kazi Ngoma Africa band aka FFU watatumbuiza katika onyesho lingine kubwala "Afrika Tage" litakalofanyika mjini Freudenstadt,kusini mwa Ujerumani,ambako nako kutakuwa na pata shika nguo kuchanika kati ya washabiki na "Bongo Dansi".FFU pia wameongeza Dozi la nguvu katika kambi yao http://www.ngoma-afrika.com/ ambako nyimbo za "Rushwa ni adui wa haki" na lile sebene la "Amiri Jeshi Mkuu" zinaweza kusikika.Zogo la "Baba wa kambo" bado linaendelea at http://www.ngoma-africa.com/ jipe raha mwenyewe

Post a Comment

0 Comments