UFAFANUZI KUHUSU UCHAGUZI WA VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB (VILLA)

1. UTANGULIZI.

Hivi karibuni kumekuwa na maelezo mbalimbali katika vyombo vyahabari kuhusu uchaguzi wa Klabu ya Villa na wanachama wengine wa Shirikisho laMpira wa Miguu Tanzania (TFF). TFF inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao kuhusuuchaguzi huo na chaguzi nyingine za wanachama wa TFF. Kila mwombaji uanachama wa TFF hana budi kutimiza mashartiyalivyoainishwa kwenye Katiba ya TFF ili kuwa mwanachama wa TFF.

Kati yamasharti hayo ni Tamko la kimaandishi kuwa anakubali kufuata Katiba ya TFF,Kanuni na maagizo katika muundo wake wa sasa na mabadiliko ya baadae na maamuziya FIFA, CAF, CECAFA, TFF na vyombo vyake (Ibara ya 7(2)(c) na Tamko kwambaatahakikisha kwamba Katiba ya TFF inaheshimiwa na wanachama wake na mtu yeyotemwenye mahusiano naye (Ibara ya 7(2) (d). Baada ya kutimiza masharti yote ya maombi ya kuwa mwanachama, kilamwanachama wa TFF anawajibika, pamoja na kutimiza masharti na matakwa mengine yakikatiba: Kuwa mwaminifu na mtiifu kwa TFF kwa maana ya kutofanya vitendovinavyokwenda kinyume na matakwa ya TFF kama ilivyoanishwa kwenye Ibara ya 12(1) (b). Kufuata Katiba, kanuni, maagizo na maamuzi ya FIFA, CAF, CECAFA naTFF. (Ibara ya12 (1) utokuwa na uhusiano wowote wa kimichezo na wanachamawaliosimamishwa au kufukuzwa. Kutimiza wajibu wowote unaotokana na Katiba, Kanuni, maagizo namaamuzi ya TFF.

(Ibara ya12 (1) (n).

Kutopeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama ya kawaida yaSheria. (Ibara ya12 (2) (e).

Mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa viongozi wa TFF na wa wanachama wote wa TFF yamekasimiwa kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa mujibu wa Katiba yaTFF Ibara ya 49 (1). Kanuni za Uchaguzi za TFF na wanachama wake zimetungwa nakuidhinishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF Ibara ya34(k).

2. MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VILLA SQUAD FOOTBALL CLUB

Klabu ya Villa ni mwanachama wa TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFFIbara ya 5 (3) na 6(5). Katiba ya Villa Ibara ya 1 (6) inatambua Mamlaka ya TFF. Ibara hiyoinasomeka hivi: “Klabu ya mpira wa miguu ya Villa Squad ni mwanachama wa TFF,itaheshimu katiba, kanuni, maagizo na maamuzi ya TFF na kuhakikisha kuwazinaheshimiwa na wanachama wake”.

Pamoja na matakwa hayo hapo juu, Katiba ya Villa katika kuzingatiauanachama wa Villa kwa TFF inazingatia pamoja na matakwa mengine haya yafuatayokama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Villa: Ibara ya 11: Wajibu wa wanachama wa Villa; Kila mwanachama wa Klabuya Mpira wa miguu ya Villa Squad atakuwa na wajibu ufuatao zaidi ya uleuliotajwa kwenye Kanuni za Asasi: Ibara ya 11 (1) (c): Kukubali kufuata Katiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi yaKlabu ya miguu ya Villa Squad na TFF. (Ibara ya 11 (2) (b)): Kutopeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama yakawaida ya Sheria.

Ibara ya 25:Mtu yeyote anayegombea nafasi yoyote ya Klabu ya mpirawa miguu ya Villa Squad hana budi kutimiza masharti yafuatayo: 1. Awe na uzoefu wa uendeshaji mpira wa miguu uliothibitishwa.2. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya kupewauchaguzi wa kulipa faini.3. Awe na umri angalau kuanzia miaka 18.4. Awe anajua kusoma na kuandika na awe na elimu ya msingi hadi sekondari.5. Awe na cheti cha elimu ya msingi na sekondari. Katiba ya Villa, kama zilivyo katiba za wanachama wa TFF inatambuamamlaka ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Ibara ya 40(5) ya Katiba ya Villainasomeka: Kamati hii itafanya kazi chini ya kamati ya uchaguzi ya TFF.

Kwa kuzingatia wajibu wake wa kikatiba kama ilivyoainishwa hapo juu,TFF iliiagiza Klabu ya Villa kuanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Klabu yaVilla kuanzai tarehe 02 Mei 2011 kwa barua yenye Kumbukumbu Na.TFF/ADM/EC11./09 ya tarehe 30 Aprili 2011 na pia kuagiza kuwa uchaguzi huoufanyike kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na ukamilikekabla ya tarehe 20 Juni 2011.: Baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Villa kukamilisha zoezi la usaili, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa barua yenye kumbukumbu Na. TFF/ADM/EC.11/17 ya tarehe 06 Juni 2011 iliiomba Kamati ya Uchaguzi ya Villa kuwasilisha taarifa yamchakato wa uchaguzi, ikitimiza majukumu yake ya kikatiba na kikanuni yakutathmini na kusimamia uchaguzi wa wanachama wa TFF. Baada ya kupata taarifa kutoka Kamati ya Uchaguzi ya Villa, Kamatiya Uchaguzi ya TFF ilifanya kikao na Kamati ya Uchaguzi ya Villa katika makaomakuu ya Klabu ya Villa hapo tarehe 08 Juni 2011, ili kupata ufafanuzi wa kinakuhusu uzingatiaji wa Kanuni za Uchaguzi na kujadili matayarisho ya uchaguzi ilikuhakikisha kama mahitaji yote ya kufanikisha uchaguzi uliokuwa umepangwakufanyika tarehe 12 Juni 2011 yamekamilika.

Kwa kuwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF haikuridhika na maelezoyaliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya Villa kuhusu matokeo ya usaili wa wagombeana vielelezo vilivyotajwa na Kamati Uchaguzi ya Villa kuwapitisha baadhi yawagombea uongozi, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa barua yenye kumbukumbu Na.TFF/ADM/EC.11/18 ya tarehe 09 Juni 2011 iliiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villauwasilishe TFF nakala za fomu za kuomba uongozi za waombaji uongozi wotewaliopitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Villa, zikiwa zimeambatanishwa na nakalaza uthibitisho wa sifa za wagombea uongozi, kwa mujibu wa Ibara ya 10 ya Kanuniza Uchaguzi za wanachama wa TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliagiza kufanyikahivyo kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26 (2)inayoipa mamlaka Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuingilia mchakato wa uchaguzi wawanachama wa TFF wakati wowote ule kuangalia na kuthibitisha usahihi wamchakato, kuhakiki na kujiridhisha kwamba Kanuni za Uchaguzi, matakwa ya Katibaya mwanachama wa TFF, Katiba ya TFF na FIFA yanazingatiwa. Kamati ya Uchaguzi ya TFF, katika kikao chake kilichofanyika tarehe10 Juni 2011 kupitia fomu za maelezo ya wagombea uongozi wa Klabu ya Villa nanyaraka za uthibitisho wa sifa za wagombea uongozi, ilibaini kuwa wagombeaBw.Mohamed Kea Mohamed, Bw. Ramadhani Soud Iddi, Bw. Alwan Mohamed Geyash, Bw. AliMohamed Daddy Baucha, Bw. Ally Ahamed Mpemba Bw. Said Yusuf Chacha, Bw. IddMohamed Mbonde na Bw. Abdalla D. Majurah hawakidhi sifa za wagombea uongozikama zilivyoainishwa kwenye ibara ya 25 (5) ya Katiba ya Klabu ya Villa. Kwakutotimiza masharti na sifa za uongozi kwa mujibu wa Katiba ya Villa, Kamati yaUchaguzi ya TFF iliwaondoa katika orodha ya wagombea uongozi kwa nafasiwalizoomba kugombea. Kamati ya Uchaguzi ya Villa ilitaarifiwa maamuzi hayo yaKamati na kuagiza uchaguzi wa Klabu ya Villa Squad utafanyika kama ulivyopangwatarehe 12 Juni 2011, kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati yaUtendaji na kwamba nafasi ya Mwenyekiti haina mgombea na itajazwa baadaye kwamujibu wa Katiba ya Klabu ya Villa Squad Ibara ya 28(c), yaani kwenye uchaguzimdogo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uonaofuata baada ya uchaguzi. Kamati yaUchaguzi ya Villa ilitakiwa kwa barua ya TFF yenye kumbukumbu EC/TFF/06/2011/002ya 10 Juni 2011kutekeleza maamuzi hayo ya TFF. 3.

KUTOFANYIKA UCHAGUZI WA VILLA

Kutofanyika kwa uchaguzi wa Villa ni ukiukwaji wa maagizo na maamuziya TFF na ukiukwaji wa Katiba ya Villa na TFF. Kuahirisha uchaguzi wa Villa kulikofanywa na mkutano mkuu wa Villani kukiuka Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10 (6) inayokatazakubadili tarehe ya uchaguzi au kufuta uchaguzi ambao umekwisha tangazwa naKamati ya Uchaguzi bila idhini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Kutoiruhusu Kamati ya Uchaguzi ya TFF ni kukiuka matakwa ya Katibaya TFF Ibara ya 49(1) inayoipa mamlaka Kamati ya Uchaguzi ya TFF kusimamiachaguzi za wanachama wa TFF. 4.

KUBADILI KATIBA BILA IDHINI YA TFF Kitendo cha kubadili Katiba ya Villa katika mkutano mkuu wa uchaguzini kukiuka Katiba ya TFF Ibara ya 12 (1)(b) na (c).

Kubadili vifungu vya Katiba ya Villa na kuweka vipengelevinavokinzana na Katiba ya TFF ni kukiuka Kanuni za Uchaguzi Ibara ya 6(a) na(b) na Katiba ya TFF ya 12 (1) (d) na (e). Mabadiliko ya Katiba ya Villa yaliyofanywa na tarehe 12 Juni 2011hayatatambulika na TFF. 5.

KUFANYIKA KWA UCHAGUZI WA VILLA ULIOAHIRISHWA KIMAKOSA.

TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villakutoendelea na vitendo vya ukiukwaji wa Kanuni za uchaguzi.

TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villakutekeleza maagizo na maamuzi ya TFF mapema iwezekanavyo kwa kukamilishamchakato wa uchaguzi kama ilivyoelekezwa na TFF. TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villakuhakikisha kuwa inakamilisha mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni zaUchaguzi za wanachama wa TFF na kupata viongozi kabla ya Kikao kijacho chaKamati ya mashindano ya TFF ambacho kitafanya maamuzi stahiki ya ushiriki waKlabu ya Villa katika Ligi kuu, endapo Klabu ya Villa haitatekeleza majukmu yakeya kikatiba kwa taratibu zilizowekwa na TFF. Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villa wanaagizwakutekeleza maagizo hayo hapo juu ili kuepuka hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidiyao na Klabu ya Villa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF na Katiba ya TFF,CECAFA, CAF na FIFA, endapo hawatatekeleza maamuzi ya TFF. 6. UCHAGUZI WA VIONGOZI WA WANACHAMA WA TFF

TFF inasisitiza kuwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF itaendelea namajukumu yake ya kusimamia chaguzi za wanachama wa TFF na inawataka wanachamawote wa TFF kuendelea kuzingatia Katiba (zinazoendana na Katiba ya TFF) naKanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na za TFF katika michakato ya uchaguzi waviongozi wao.

Angetile Osiah

KATIBU MKUU

Post a Comment

0 Comments