HARAMBEE YA MAENDELEO YA ELIMU, MAJI NA AJIRA, MKOA WA TABORA NA MJINI MAGHARIBI

Mhe. Balozi Seif Ali Idd (MBM) – Makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, akipeana mkono na Aden Rage – Mbunge wa Jimbo la Tabora na Mwenyekiti Club ya Simba, kulia kwake ni Mhe. Eng. Athuman R. Mfutakamba – Naibu Waziri wa Uchukuzi.
Mhe. Dkt. Hussein A. Mwinyi – Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akitangaza jumla ya michango aliyopokea kwa wadau wakati wa harambee ya Elimu, Maji na Ajira, Tabora na Mjini Magharibi kulia ni Mama Asha Seif – Mke wa Makamu wa pili wa Rais, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kushoto kwake ni Ndugu Hassan Wakasuvi - Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tabora.

Wa pili kulia ni Mhe. Balozi Seif Ali Idd (MBM) – Makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulia kwake ni Mhe. Eng. Athuman R. Mfutakamba – Naibu Waziri wa Uchukuzi akipeana mkono na Mama Asha Seif – Mke wa Makamu wa pili wa Rais, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kuchangia wakati wa harambee ya Elimu, Maji na Ajira, Tabora na Mjini Magharibi.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA TABASAMU PR CONSULTANCY.

Shughuli ilikuwa ni Harambee (Fundraising) ya maendeleo ya Elimu, Maji na Ajira mkoa wa Tabora na Mjini Magharibi siku ya tarehe 4/6/11 ambapo waheshimiwa Wabunge na Viongozi wa Mikoa ya Tabora na Mjini Magharibi - Zanzibar, waliunga mkono jitihada za serikali mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapatia huduma muhimu wananchi katika sekta za Maji, Elimu na Ajira. Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Balozi Seif Ali Idd (MBM) - Makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Jumla ya million 631,175,000 (ahadi na fedha taslim) zilikusanywa usiku huo wakati fedha taslim kati ya zilizokusanywa ni million 3,600,000/= .

Post a Comment

0 Comments