Na Ripota Wetu, Dar es Salaam
Kulia ni Waziri wa Wizara ya Fedha Mustafa Mkulo.
SIKU chache baada ya Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo kuwasilisha bajeti ya Serikali Bungeni mjini Dodoma, Viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati wamewataka Wabunge wote kutoipitisha Bajeti hiyo kwani haina manufaa kwa watanzania.Wakichangia mjadala wa kuichambua bajeti hiyo ulioandali na Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), uliofanyika jana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, alisema bajeti hiyo imejaa upotoshaji na kiini macho kwa wananchi.Profesa Lipumba, alisema vipaumbele vilivyowasilishwa Bungeni na Serikali vinakwenda kinyume na hali halisi ya matumizi ya Serikali ambapo zaidi ya asilimia 53.6 ya fedha imetengwa kwa matumizi mengine.
Aidha alisema kitendo cha Serikali kutanguliza kipaumbele cha umeme kinakwenda kinyume na azimio la kilimo kwanza huku sekta hiyo muhimu Wizara yake ya Kilimo ikitengewa asilimia 3.4 ya fedha hali inayoweza kuathiri uzalishaji wa mazao.“Kuna umuhimu wa kufanya mjadala wa kitaifa kuhusu bajeti kabla haijawasilishwa Bungeni huwezi kuwa na bajeti ya Trioni 13.5 huku ukitenga asilimia 14 kulipa madeni na Tririoni 11 ndizo zikaendesha nchi hakika hii bajeti haina tofauti na ya mwaka uliopita.“Hii ni hatari kubwa kwa Serikali iko tayari kuwasomea bajeti nchi wahisani kuliko watanzania bajeti ya Sekta ya afya imekuwa ikishuka kila mwaka hadi kufikia Tririoni 1.2 ikiwa tofauti na mwaka uliopita ya Trioni 1.209 huku ni kuuweka rehani maisha ya Watanzani wanaotegemea hospitali zetu za ndani” alisema Profesa Lipumba.Profesa Lipumba, ambaye kitaalamu ni Mchumi, alizidi kuichambua Bajeti hiyo na kusema kuwa kwa mujibu wa Waziri Mkulo, amewadanganya Watanzania ambapo inaonyesha kuwa Mtanzania anayetumia sh. 641 na anaishi chini ya Dola moja inaonyesha kuwa sio maskini hali hali ya kuwa maisha yanazidi kuwa magumu.
Akizungumzia kukua kwa deni la Taifa ambapo deni limeongezeka na kufikia asilimia 7 sawa na Tririoni 5.4 ikiwa tofauti na mwaka uliopita la Dola za Marekani Bilioni 1 na Milioni 500.Alisema Bajeti hiyo imekuwa si ya heshima huku ikiwasahau wastaafu kuhusu kulipwa mafao yao ambapo kwa sasa imekuwa tofauti na kinyume na dira ya Taifa kwa watu wote.
Profesa Lipumba, alionya juu ya mpango wa Serikali wa kuwa na dira ya Taifa ambao hautoi tija kwa watu wake ambapo aliitaka Serikali kuitisha mjadala wa kitaifa ili kuweza kupanga upya dira hiyo itakayo shirikisha watu wote nchini.“Sina hakika kama Rais Kikwete, ameusoma mpango huu wa dira ya Taifa kwa haulezi kwa kina matatizo ya Watanzania kitendo cha Waziri Mkulo kushindwa kuileza dira ndani ya bajeti hakika ni tatizo kwa nchi yetu na siasa zimetawala katika masuala ya kitaalamu” alisema Profesa Lipumba.Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi huru ya uchumi na kijamii Dk. Bohela Lunogelo, alijikuta katika wakati mgumu hasa mara baada ya kusifu mpango wa Serikali kuhusu matumizi ya pikipiki za kubebea wagonjwa za matairi matatu.Hata hivyo mara baada ya kukutana na zomea zomea hiyo alilazimika kujitetea na kusema alikuwa akitoa mfano wa matumizi ya pikipiki hali ya kuwa bajeti ni moyo wa Taifa.
Dk. Lunogelo, alisema kutokana na hali matarajio ya Watanzania ni makubwa kwa Serikali yao na kuvitaka vyama vya siasa kuwa na utaratibu wa kukosoa na kujibu hoja kwa kufikisha ujumbe kwa wananchi wa Vijijini.“Ni vizuri bajeti ikawa inajadiliwa na Watanzania mapema alau kwa muda wa miezi sita kabla ya kufikishwa Bungeni na hapa … Bajeti itakuwa inatafsiri sasa ya kuandaliwa na Watanzania wote” alisema Dk. Lunogelo.
Hamadi Tao
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Hamad Tao, alip[inga kitendo cha Serikali kutenga sh. Bilioni 432 kwa ajili ya Wizara ya Ulinzi ili kununulia silaha hali ya kuwa Watanzania wanakabiliwa na njaa.“Ninapinga na kulaani kwa nini Wizara ya Ulinzi itengewe bilioni 432 kwa ajili ya kununulia silaha huku watu wakiwa wanakufa kwa njaa, kwani nchi ipo kwenye vita kwa hili ni kuwadhihaki wananchi wa Taifa hili” alisema Tao.
MbatiaKwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema umefika wakati kwa Chama Cha Mapinduzi kutambua kuwa Watanzania wa zamani sio wa leo.
“Umefika wakati CCM na watawala kutambua nchi ni ya kwetu wote kutambua Bajeti ni watanzania wote na si ya Serikali pekee na viongozi wake, na yanahitajika mawazo mapya kwa maslahi ya Taifa” alisema Mbatia.Mbatia mambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa mjadala huo alikionya Chama Cha Mapinduzi kwa kusoma nyakati nna sura ya watanzania wa sasa nini wanahitaji ndani ya nchi yao.
Kwa upande wake Allan Mwaigaga, aliyejitambulisha ni mwananchi kutoka mkoani Mbeya, alisema umefika wakati wa kufanya vitendo kuliko maneno kwa kuwaweka kando waovu wanaoliumiza Taifa.
“Mwalimu Nyerere, alipoondoka aliacha Viwanda hapa nchini kila kona na leo tunahamasishwa mradi wa EPZ huku bajeti ikishindwa kueleza namna itakavyoweza kufufua na kujenga viwanda vikubwa na vidogo hakika hili Wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao wasiipitishe bajeti hii na ilirudishwe kwa wananchi ili ijadiliwe kwa kina” alisema Mwaigaga.
Erasto TumboNae Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA Erasto Tumbo, alisema umefika wakati kupunguza matumizi yake makubwa huku akiitaka Wizara ya Fedha kuacha kutenga fedha za tafrija na ukarabarti wa Ikulu kila mwaka.Alisema kitendi cha Ikulu kutengewa kiasi kikubwa cha fedha huku wananchi wakikosa dawa hospitali ni kukosa uzalendo na umakini kwa viongozi hali inayowafanya wananchi kukata tama ya maisha.Mbunge wa Ziwani (CUF) na hoja binafsiKatikati ya mjadala huo Mbunge wa Jimbo la Ziwani Mohamed Zuberi Ngwali (CUF), alisema umefika wakati wa kujadili fedha za Umma na hata nafasi ya wabunge wa viti maalum, ambao hawana kazi kubwa kuliko wabunge wa majimbo.Alisema katika kuhakikisha nasimamia fedha za Umma yupo mbioni kuwasilisha hoja binafsi Bungeni kwani wabunge hao hawafanyi kazi kubwa zaidi ya kununua hereni za dhahabu na Magauni wawapo Bungeni.
“Nitawasilisha hoja binafsi ili kuhoji nafasi na kazi za wabunge wa Viti maalum Bungeni … sisi tupo wawakilishi wa majimbo tuliochanguliwa wao wana kazi gain” alisema na kuhoji Mbunge huyo.Hata hivyo hadi mwisho wa mjadala huo washiriki hao waliipinga bajeti hiyo na kuwataka Wabunge wote bila kujali vyama vyao kutoipitisha bajeti hiyo kwani haina jipya kwa maisha ya Watanzania.
0 Comments