ANGETILE, WAMBURA WAULA TFF

Mandishi mkongwe nchini , amabye pia ni mmoja kati ya Wahariri Mahiri wa Michezo na Burudani Tanzania ,Angetile Osiah, amechukua nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Shurikisho la Soka nchini (TFF), baada ya kutangazwa na Kamati ya Utendaji ya TFFmara baada ya kuomba nafasi hiyo .

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Osiah amesema amefurahi kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa TFF hivyo nafasi aliyoipata ataitumia kwa faida ya wananchi ili maendeleo yaweze kupatikana na kuendeleza soka nchini.

Amesema ni changamoto nyingi zinamkabili pindi atakapokuwa katika kazi yake lakini yupo tayari kukabiliana nazo,Angetile ama kwa jina la utani 'Ngeta' anategemea kuanza kazi mapema Januari mwakani.

Wakati huohuo Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), imemtangaza Boniface Wambura kuwa msemaji wa TFF mara baada ya kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
Wambura amechukua nafasi hiyo ambayo awali ilikuwa ya aliyekuwa msemaji Florian Kaijage aliyesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kufanya kazi yake kama ilivyotakiwa wakati wa mechi za Kimataifa kati ya Tanzania na Morocco ambapo wimbo wa Taifa haukusikika kwa ufasaha siku hiyo huku mgeni rasmi akiwa Rais Jakaya Kikwete.

Post a Comment

0 Comments