Meneja wa Huduma za Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mhandisi Andrew Kisaka akitoa mada kwenye mafunzo ya Wanablogu Tanzani Bloggers Network (TBN),kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 20295 uliofanyika Makao Makuu ya TCRA.
Mhandisi Kisaka amesema kuwa kwa niaba ya TCRA,.wanakemea maono yanayotolewa na baadhi Viongozi wa dini ambao wanajita Manabii na Mitume kwa kutabiri vifo kwa viongozi waache mara moja.
"Kauli hizi za maono yao kuhusu vifo vya Viongozi na wagombea katika ngazi mbalimbali zinaogofya wananchi hivyo tunatarajia watatumia nafasi zao za kuwa viongozi wa dini katika kudumisha amani na siyo kutoa utabiri unaoleta taharuki kwa jamii ya watanzania wasivuke mipaka yao kwani sheria ina mkono mrefu" amesema Mhandisi Kisaka.
Wakati huohuo Uongozi wa Tanzania Bloggers Network N) umekemea vikali tabia hiyo ambayo imeonekana kushamiri kwa kasi ambapo kumekua na baadhi ya Viongozi wa sini kutoa utabiri nahata pindi kifo kinapotokea wamekua wakisisitiza kwamba walitabiri jambo ambalo halifai katika jamii.
Aidha kwakaulimoja Mabloga hao wameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na utoaji wa kauli hizo ambazo zinaweza kuletamachafuko nchini kama hawatadhibitiwa mapema.Bi Rehema Mpagama kutoka Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, amewasilisha mada ya Maadili na Sheria kwa Waandishi wa Habari.
Mafunzo hayo yameratibiwa na TCRA, yalilenga kuwaandaa Mabloga kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu.
Pamoja na mada ya ulinzi wa taarifa binafsi, mada nyingine muhimu zilizotolewa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uchaguzi na Matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika uandishi wa habari.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuongeza uwezo wa mabloga kuhakikisha wanafuata sheria na maadili ya uandishi, jambo linalotazamiwa kuchangia mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu.Aidha mtoa mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC),Innocent Mungy sheria hiyo inakataza mtu kuzungumziwa kuhusu afya yake, mwenendo, au taarifa zake binafsi kutolewa bila ridhaa yake. Mungy alisisitiza kuwa sheria hii ina adhabu kali na lazima ifuatwe na kila mtu, si tu mabloga na waandishi wa habari.







0 Comments