TBN "TUNAISHUKURU WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI, ,SANAA NA MICHEZO ""

"Tanzania Bloggers Network  TBN tunatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri  ya 

Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi mahiri wa Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kutoa uwajibikaji  wanablogu katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 .

Shukrani hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe  leo tarehe  11 Agosti  katika mafunzo  hayo ya siku moja   yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano  wa Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania TCRA ,Makao Makuu Jijini Dar es Salaam. 

"Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya dhati ya Rais Samia ya kuwa na taifa tulivu na lenye maendeleo ambapo habari sahihi na zenye uwajibikaji ndiyo nguzo kuu" amesema Msimbe.

Tunatoa shukrani za kipekee kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Katibu Mkuu wake, Ndugu Msigwa, kwa kuona umuhimu wa TBN na kuwezesha mafunzo haya pia shukrani hizi  ziende kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuandaa na kuratibu mafunzo haya muhimu ambayo yanalenga kutuandaa mabloga kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi  na  uadilifu.

"Tunawashukuru wakufunzi wote ambao wamejitolea kushiriki na kutupa elimu muhimu kuhusu Mwongozo wa Waandishi wa Habari, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi, maadili na sheria.

Historia ya blogu ilianza nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000 blogu zilibadilika kuwa njia kuu za kupokea na kutoa maudhui ya aina mbalimbali, zikiwa ni zana muhimu za kufikia umma, kubuni maoni, na kusambaza habari na matukio. 

"Mafunzo haya ni fursa kubwa kwetu kutoa taarifa sahihi na zenye uwajibikaji, jambo muhimu katika kujenga mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu" amesema Msimbe.

Mtandao wa Wana Blogu wa Tanzania (TBN) ni jamii yenye nguvu ya waendesha blogu wa Kitanzania walio ndani ya nchi pamoja na walio katika Diaspora.

 Ulimwengu wa blogu umekua kwa kasi na blogu mpya inazaliwa kila sekunde, ikichangia katika hadithi inayobadilika ya jamii yetu" amesema Msimbe.

TBN iliundwa rasmi Aprili 2, 2015, chini ya Sheria ya Tanzania ya Mashirika (CAP. 337 R.E. 2002) na kupata Cheti cha Usajili namba S.A. 20008 cha Tarehe 02 Aprili, 2015 kutoka kwa Msajili wa Taasisi zisizo za Kiserikali katika Wizara ya Mambo ya Ndani. Uanachama wake wa awali ulianza na watu 100, ambapo baadaye walifikia 320. Makusudio mama yalikuwa ni kupanua TBN ili ijumulishe wanachama 1,000 wenye shughuli ndani na nje ya nchi miaka ijayo. Masharti ya kuwa mwanachama ni kuwa na blogu yenye uhai usiopungua umri wa miezi sita.

Dkt. Egbert Mkoko, Mhadhiri  katika Shule Kuu ya Uandishi  wa Habari  na Mawasiliano ya Umma (SJMC), amewasilisha  mada ya  katika  Uandishi wa Habari za Uchaguzi  na kusisitiza Mabloga, Waandishi  wa Habari  kuzingatia  kulenga uelewa  kwa wapiga kura ,uwajibikaji  kisiasa  na kudumisha demokrasia  na kuepuka kueneza uvum na kuto nunuliwa na takrima .

"Kwa miaka mingi, Mtandao wa Mabloga Tanzania (TBN) umekuwa sauti muhimu katika jamii yetu. Tumekuwa jukwaa huru linalowapa Watanzania fursa ya kutoa mawazo yao, kushiriki uzoefu, na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu jamii yetu. Jukumu letu si tu kutoa habari, bali pia kuhakikisha habari hizo ni sahihi na zinazingatia maadili na utamaduni wa Kitanzania" amesema  Msimbe. 

 Amesema kuwa bloga wote  wanapaswa kulaani vikali wale wote wanaokwenda kinyume na maadili yetu, wanaosambaza habari za uongo na za uchochezi.

"Wakati tunasikiliza mada mbalimbali tunatakiwa kuwa makini kusikiliza na kudadavua huku tukiweka akilini kwamba Blogu, kwa kuwa zinazalisha kiasi kikubwa cha maandishi (text-based content) kinachoakisi uhalisia wa Tanzania kutoka mitazamo mbalimbali, zinatoa ‘malighafi’ muhimu kwa Akili Mnemba. Kadiri wanablogu wanavyoandika kuhusu mambo mbalimbali ya kitaifa – siasa, uchumi, utamaduni, maisha ya jamii, changamoto, na mafanikio – ndivyo tunavyojenga hifadhidata kubwa na tajiri ya taarifa sahihi na za kisasa kuhusu Tanzania" amesema Msimbe.

"Hii inamaanisha kuwa AI inapata fursa ya kujifunza kutoka vyanzo halisi vya Kitanzania. Wakati watu kutoka nje ya nchi wanapotaka kujua "Tanzania ikoje?" au wakati AI inahitajika kutoa taarifa muhimu kuhusu nchi yetu, itakuwa na uwezo wa kutoa majibu sahihi zaidi, yenye kina, na yanayoakisi hali halisi kwa sababu imefunzwa kwa maudhui mengi na tofauti kutoka kwenye blogu zezetu.

Amesema kuwa 

Bloga wanapaswa kuchakata  habari sahihi vivyo hivyo wanatakiwa kuwa na uhakika  iwe kwa kutumia AI au la.

"Inapaswa kukumbuka kuwa ingawa AI inaweza kuwa zana yenye nguvu; hisia za kibinadamu, uzoefu halisi, na mtazamo wa kipekee wa mwanablogu ndio unaoleta uhai na uhalisia katika maudhui. AI hawezi kuchukua nafasi ya ubunifu wa mwanadamu na uwezo wetu wa kuhisi na kufahamu matukio kwa undani. Kwa hiyo, tunapaswa kuitumia AI kama msaidizi, na si kama mbadala.

Wakati huohuo Bloga wametakiwa kuwa waangalifu na zana mbalimbali za kutengeneza maudhui kwenye habari zao kabla ya kuziweka kwenye  kurasa zao.

" Tunamhakikishia Mhe.Rais Dkt. Samia kwamba tupo pamoja naye katika juhudi za kudumisha amani na utulivu. Tutaendelea kutumia majukwaa yetu kuandika na kusambaza habari za maendeleo zinazoakisi juhudi za Serikali katika kujenga Tanzania mpya" amesema Msimbe.

Tunaamini kwa mafunzo ya leo mabloga watawezeshwa kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, na uwajibikaji. Kwa pamoja, tunaweza kujenga Tanzania yenye habari sahihi, yenye uwazi, na yenye uwezo wa kujadiliana na kuingia katika uchaguzi salama kwani kuna maisha kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

"Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Mungu Ibariki Tanzani"amehitimisha  Msimbe.

Post a Comment

0 Comments