Aliyekuwa Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama amefariki Dunia leo leo tarehe 11 Desemba, 2025 Jijini Dodoma.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu kupitia taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma Ofisi ya Bunge, Dodoma leo Desemba 11, 2025.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutangaza kifo cha Mbunge wa Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kilichotokea leo 11 Desemba, 2025 Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Peramiho, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mhe. Spika.
“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina.” — imesema taarifa hiyo.

0 Comments