Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt.Mawazo Nicas ametoa siku saba kwa mfugaji wa Nguruwe kujenga shimo kutiririsha maji na kinyesi cha wanyama hao wanaofugwa kwenye eneo la watu bila ya kuzingatia usafi wa mabanda yake.
Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kutoa malalamiko yao kwamba wanapata kero ya harufu mbaya maji na kinyesi vyote kutapakaa mtaani hapo kama hiyo haitoshi pia imeelezwa kuwa mmiliki huyo pia anachinja Nguruwe hao hapohapo.
Malalamiko hayo yametolewa leo mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas alipokua akisikiliza kero za wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Kongowe leo 5 Januari 2025.
" Suala la Nguruwe ni kweli lipo Mstahiki Meya nimeshuhudia kuona mmiliki akiwa hajajenga uzio na mazingira ni machafu tumekuta kinyesi kimetapakaa na maji vyote vikitiririka kwenye makazi ya watu jambo ambalo limekua likilalamikiwa kwa muda mrefu na muhusika amepewa maonyo mengi na uongozi wa Serikali ya Mtaa lakini hajawahi kutekeleza hivyo basi nampa wiki mbili ili aweze kujenga shimo la kupokelea kinyesi cha Nguruwe pia tumemweleza kesho tarehe 6 Januari 2025 afike katika Ofisi za Serikal ya Mtaa Kongowe kwa kikao maalumu" amesema Afisa Mtendaji Kata Vicent Paul Tozzo Serikali ya Mtaa.
Tozzo amesema kuwa endapo muhusika atatekeleza maelekezo aliyopewa atapigwa faini kwa mujibu wa Sheria za mifugo,pia atalazimika kuhamisha mifugo hiyo katika eneo la makazi ya watu.
Dkt. Nicas amesema kuwa baada ya siku saba atarudi kumkagua kama ametekeleza maelekezo aliyopewa ,nasema hivi kwa sababu watu wanatakiwa kuishi huku wakitabasamu hii ni nchi yetu sote hakuna anayeishi juu ya Sheria.


.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 Comments