WATAFITI WAUNGANISHWA NA WAANDISHI WA HABARI, EGPAF NAO WANENA JUU YA ELIMU YA KUPIMA HIV


Rais wa Tanzania Health Summit, Dkt Omary Chilo (kulia) akipeana  mkono na Mkurugenzi wa ResearchCom, Dkt. Syriacus Buguzi baada kumaliza kuzindua ushirkiano wa mawasiliano ya kisayansi wakati wa mkutano wa mawasiliano ya kisayansi  utakaowawezesha wanasayansi kuwasiliana kwa ufanisi. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia nyuma yao ni Sammy Awami.

Mkurugenzi wa ResearchCom, Dkt. Syriacus Buguzi akizungumza wakati wa mkutano wa mawasiliano ya kisayansi  utakaowawezesha wanasayansi kuwasiliana kwa ufanisi. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Mwandishi Mwandamizi wa habari kutoka BBC, Sammy Awami akizungumza wakati wa mkutano huo.

Afisa mshauri wa mawasiliano na uchechemuzi,  katika Shirika la EGPAF, Nuru Ngailo akizungumza na Michuzi Blog na Michuzi TV. 

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
IMEELEZWA kuwa tafiti za kisayansi ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa jamii ni muhimu zikapata nafasi ya kuandikwa kwenye vyombo vya habari .

Tukio hili la Uwasilishwaji wa Taarifa za Sayansi limefanyika leo Julai 17, 2024  jijini Dar es Salaam, kuelekea Mkutano wa 11 wa Afya wadau wa afya, yaani Tanzania Health Summit utakaofanyika mapema Oktoba, Zanzibar ambapo wataalamu kutoka mashirika mbalimbali, ya ndani na ya kimataifa, walikusanyika katika tukio la Uwasilishaji wa Taarifa za Sayansi ili kuonyesha matokeo Chanya ya kazi zao kwa jamii za Tanzania.

Mkurugenzi wa  ResearchCom Dkt. Syriacus Buguzi ,amesema mkutano huo pia utawawezesha wanasayansi kuwasiliana kwa ufanisi kuelekea Kongamano hilo la 11.

"Research Com tumeingia ubia na Tanzania Health Summit ili kujenga kwa mazingira kwa watafiti na watu wanaoendesha miradi mbalimbali waweze kuwasilisha taarifa zao za kisanyansi zenye matokeo kwenye jamii jinisi ambavyo zinaweza kubadilisha maisha ya watu"

Amesema kuwa tafiti nyingi zinashindwa kuwasaidia wananchi kwa sababu ya kutowafikia.

"Kwa muda mrefu kumekuwepo changamoto kwa watafiti au wanayansi wanapofanya kazi zao hazipati nafasi katika vyombo vya habari kwa hivyo kunakuwa na changamoto kwao katika kuwasilisha hizi tafiti"

"Sisi tumetengeneza mazingira kwa wataalamu hawa kufanya kazi na waandishi wa habari ili zile kazi zao zipate nafasi ya kufahamika kwenye jamii na kutoa matokea chanya"

 Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa mshauri wa mawasiliano na uchechemuzi,  katika Shirika la EGPAF, Nuru Ngailo amesema kuwa shirika hilo litatumia kongamano hilo kwa ajili ya kutoa elimu itakayowalenga vijana, Mama na mtoto juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi na kifua kikuu.

"Kupitia mradi wa afya yangu unaofadhiliwa na watu wa Marekani USAID , tunatekeleza mradi huu Kanda ya Kati na Kaskazini mwa Tanzania..tumefikia watu wengi mathalani kule Singida tulimfikia mtu mmoja ambaye ni kiongozi katika jamii aliyekuwa anadhana ya kuwa mwanaume kupima HIV ni udhaifu lakini siku moja alipata kuusikia ujumbe wetu kupitia mhudumu wa afya tunayefanya naye kazi alielewa juu ya umuhimu wa kupima na sasa yeye amekuwa balozi wetu ana ameweza kuwafikia watu zaidi ya 900 kwa miezi sita tu tangu amejiunga. " Amesema

Amesema kuwa mradi huo umewafikia watu katika Mikoa sita nchini Tanziania ambapo wamekuwa wakikutana changamoto kubwa inayowakabili wanajamii ikiwa ni pamoja na tamaduni na mila potofu juu ya HIV .

"Changamoto kubwa ni watu kuwa na mila au tamaduni potofu kuhusiana na kupima HIV na Kifua Kikuu" amesema Nuru.

Amesema kuwa kwa upande wa Mama anayeishi na maambukizi ya HIV akiwa ana mtoto mdogo wanatoa elimu juu ya kumlinda mtoto kuanzia kipindi cha ujauzito mpaka anazaliwa ili mtoto azaliwe salama.

Akizungumzia juu ya takwimu za za wagonjwa tokea mradi huo ulipoanza Oktoba 2021 hadi Machi 2024, Meneja Mwandamizi na Ufuatiliaji wa Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation (EGPAF) Frank Lyimo amesema mpaka sasa watu 1,608,798 walipimwa HIV ambapo kati yao watu 41,482 walikutwa wameathirika na watu 50,266 walinzishiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments